Katikati ya harakati za Qur’an: Mashindano ya Qur’an ya vikundi awamu ya tatu yaingia hatua ya pili..

Maoni katika picha
Kikosi kinacho shiriki mashindano ya Qur’an ya vikundi yanayo simamiwa na kituo cha kuandaa wasomi na mahafidhi chini ya Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya kimekamilisha hatua ya kwanza ya mashindano hayo, ambapo vikundi 16 wamepata max za juu katika vikundi 24 walio shiriki mashindano haya, kulikua na ushindani mkali sana, mashindano yanafanyika kila siku katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s).

Hatua hii ilikua na ushindani mkubwa na matokeo yalikaribiana sana, hatua ya pili ndio ya mwisho inatarajiwa kufikia kilele chake usiku wa mwezi kumi na tano ambao kutakua na kumbukumbu ya kuzaliwa kwa imamu Hassan (a.s).

Kumbuka kua kila kikundi kinaundwa na watu watatu (msomaji, haafidh na mfasiri) kutokana na utaratibu wa mashindano, yalifunguliwa kwa kuwakutanisha kikundi cha Muthanah na Diyala, na yanaendelea kwa muda wa siku 15, kila siku vinashiriki vikundi vinne, wanaulizwa mashali mbalimbali, jopo la majaji linaundwa na majaji wanne ambapo wanaangalia hukumu za tajweed, sauti, naghma, tafsiri, mada, kusimama na kuanza pamoja na hifdhu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: