Usajili unafanyika siku za Juma Pili na Juma Tano katika kila wiki ndani ya kipindi chote cha mwezi mtukufu wa Ramadhani na wiki mbili baada ya Ramadhani, usajili unafanyika katika kitongoji cha Baladiyya ndani ya jengo la Raudhat Saaqi, na masomo yataanza tarehe (22/07/2017 hadi 14/09/2017), katika kituo cha masomo cha Ameed kitongoji cha Baladiyya shule ya msingi Ameed ya wasichana na Saaqi ya wavulana.
Kitongo kimeeleza baadhi ya mambo muhimu:
- 1- Shule itafundisha masomo muhimu ya sule za msingi darasa la sita kwa ajili ya kuwajengea uwezo.
- 2- Shule itafundisha kwa mujibu wa ratiba na silabasi inayo fatwa katika vituo vya elimu vya Ameed.
- 3- Shule itaandaa matukio ya kielimu na kimalezi pamoja na mashindano ya michezo na matukio ya burudani.
- 4- Shule itagharamia usafiri wa kwenda na kurudi wa wanafunzi watakao sajiliwa.
- 5- Shule itatoa chakula kwa wanafunzi baada ya swala za jamaa za Duhurain.
- 6- Masomo yataanza saa mbili ashubuhi hadi saa nane na nusu mchana baada ya Dhuhurain.
- 7- Masomo yataanza siku ya Juma Mosi (22/07/2017) na yataisha Alkhamisi (14/09/2017m).