Kituo cha maarifa ya Qur’an tukufu kuifasiri na kuichapisha chini ya Maahadi ya Qur’an katika Atabatu Abbasiyya tukufu, wametangaza kuongeza muda wa kupokea washiriki wa shindano la muandishi bora kuhusu Qur’an tukufu kwa mujibu wa mafundisho ya vizito viwili, hii ni kwa ajili ya kuwapa nafasi zaidi washiriki na kuwakumbusha wale walio chelewa kushiriki katika shindano hili, ambapo siku ya mwisho ya kupokea nakala za vitabu itakua siku ya Alkhamisi (17 may 2018m).
Kumbuka kua shindano hili linalenga kueneza mafundisho halisi ya Qur’an kwa mujibu wa vizito viwili –Qur’an tukufu na kizazi kitakasifu- katika jamii za waislamu kama alivyo usia Mtume Mtukufu (s.a.w.w).