Kwa ajili ya kuwasaidia majemedari wa Hashdi Sha’abi na jeshi la serikali: Atabatu Abbasiyya yafungua kiwanda cha kutengeneza barafu katika mji wa Mosul..

Maoni katika picha
Kutokana na kuongezeka joto na kuingia mwezi mtukufu wa Ramadhani aidha kupunguza ugumu kwa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi na jeshi la serikali wanao endelea kung’oa magaidi ya Daesh katika vita ya kukomboa aridhi za Iraq zilizo tekwa, Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia kamati ya maelekezo na msaada wa kimanawiyya na kimkakati wamefungua kiwanda kinacho hamishika cha kutengeneza barafu na kukiweka chini ya usimamizi wao.

Jambo hili limefanyika ikiwa kama sehemu ya utekelezaji wa maagizo ya Marjaa dini mkuu yanayo sisitiza kuwasaidia wapiganaji kwa ajili ya kuwapa nguvu katika vita na kuhakikisha wanapata ushindi mkubwa.

Kiongozi wa kamati hiyo Shekh Haidari Aaridhiy kutoka katika kitengo cha dini ameuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Baada ya kumtegemea Mwenyezi Mungu mtukufu na taufiq yake, tumefungua kiwanda kinacho hamishika cha kutengeneza barafu katika mji wa Mosul, katika kituo cha kamati ya maelekezo na msaada wa kimanawiyya na kimkakati chini ya Ataba tukufu katika mji ulio kumbolewa wa Tal-abatwa, ukizingatia kua barafu ni muhimu sana kwa wapiganaji hasa katika kipindi hiki cha kuongezeka kwa joto”.

Akaongeza kusema kua: “Kina uwezo wa kuzalisha vipange (40) vya barafu kwa saa moja, pia tunapeleka barafu katika kituo cha msaada wa kimkakati na kuzisambaza katika mji wa Samara, kila siku tunasambaza karibu vipande vya barafu (600 -700) kutoka katika kiwanda cha Ataba tukufu na kwenda katika vituo vyote vya jeshi, upatikanaji wa barafu ni hatua nzuri inasaidia kupatikana kwa maji ya baridi kwa wapiganaji na utunzaji wa chakula, ukizingatia kua wapo majangwani ambako hawana vifaa vya umeme kama vile friji na vinginevyo”.

Tunapenda kusema kua Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kutoa misaada kwa wapiganaji waliopo katika uwanja wa vita toka kutolewa kwa fatwa tukufu hadi leo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: