Mwezi mtukufu wa Ramadhani ni msimu wa ibada na dua, miongoni mwa dua wanazo dumu nazo waumini ni zile zilizo pokelewa katika zaburi ya Aali Muhammad (a.s) Sahifatu Sajjadiyyah cha imamu Zainul-abidiin (a.s), kwa ajili ya kuangazia baadhi ya madhumuni ya dua zinazo husiana na mwezi huu mtukufu, ikiwa pia ni sehemu ya ratiba iliyo pangwa na Atabatu Abbasiyya tukufu katika mwezi wa Ramadhani, kitengo cha dini kinaendesha mihadhara ya tafsiri ya dua za imamu Zainul-abidiin (a.s) ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Mihadhara inafanywa kila siku katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), hutolewa na Shekh Ali Muhaan kutoka katika kitengo cha dini cha Atabatu tukufu, alipo kutana na mtandao wa Alkafeel alisema kua: “Mwezi wa Ramadhani ni mwezi wa kufunga, Mwenyezi Mugu mtukufu anatutaka tutekeleze ibada hiyo, kwa ajili ya kututhibitishia ubinadamu wetu katika mambo makuu ya kushikika ambayo hutufanya kua watu duni, lengo la funga ni kupandisha hadhi ya mwanadamu, kwa kuifanya roho iingize katika mwili baadhi ya matukufu yake, ili kumfanya mwanadamu apate radhi za Mwenyezi Mungu na kumfanya aishi karibu naye, hivyo kwa ajili ya kunufaika na mwezi huu mtukufu, na kuhakikisha tunafanya kazi kwa mujibu wa mafundisho ya Ahlulbait (a.s), huu ni mwaka wa tatu mfululizo tunaendesha mihadhara hii inayo endana na utukufu wa mwezi huu”.
Akaongeza kusema kua: “Katika mihadhara hii tunaelezea dua za imamu Zainul-abidiin (a.s) zilizopo katika kitabu cha Sahifatu Sajjadiyyah zinazo husu kuupokea mwezi mtukufu wa Ramadhani, zinazo anza kwa kusema: (Kila sifa njema zinamstahiki Allah ambaye ametuongoza kwa utukufu wake, tuwe wenye kushukuru ihsani zake, na kwa hilo atulipe malipo ya wafanyao mema…), imepokewa kua imamu Zainul-abidiin (a.s) ulikua ukiingia mwezi wa Ramadhani hazungumzi ispokua kwa dua, tasbihi, istighfaar na takbiir, hakika tunatilia umuhimu sana watumishi kuhudhuria mihadhara hii kwa sababu mbili, kwanza: mihadhara ni ya mtiririko inatakiwa kupatikana wasikilizaji wa kudumu, pili: tunajaribu kuwazindua watumishi na mazuwaru kuhusu umuhimu wa mwezi huu mtukufu na kuzidisha kufanya maghfira ba ibada”.