Tarehe kumi na mbili ya mwezi wa Ramadhani: ni siku aliyo unga undugu Mtume (s.a.w.w) na imamu Ali (a.s)..

Maoni katika picha
Ndani ya siku hii –tarehe kumi na mbili Ramadhani tukufu- ilikua siku ya kuunga undugu baina ya Muhajirina na Answari katika mji wa Madina Munawwarah mwaka wa 1 hijiriyya au mwaka wa pili, Mtume (s.a.w.w) alifanya tukio hilo kama hatua ya kwanza katika kujenga uhusiano wenye misingi ya kumuamini Mwenyezi Mungu na kuliwazana, undugu ambao matokeo yake yataonekana katika kuamiliana baina yao na kushikamana, kama sehemu ya kuelekea katika jamii ya kiislamu yenye mshikamano kwa ajili ya kutangaza neno la Mwenyezi Mungu mtukufu.

Jambo la kwanza alilofanya Mtume (s.a.w.w) baada ya kujenga msikiti mtukufu ni tukio la kuunga undugu, ambapo lilitangazwa katika nyumba ya Anasi bun Maalik (r.a) ambayo ilikua ikiwaunganisha Muhajirina na Answari, undugu uliojengwa katika msingi wa imani, na kielelezo cha kuthibitisha upendo, kusaidiana na kulindana, na kupeana mali na mahitaji, huo ulikua ni undugu maalumu tofauti na undugu wa kawaida wa waislamu wote, kwa sababu wale walio ungana katika undugu huo walipewa haki ya kurithiana baina yao bila kuwepo na uhusiano wa kinasaba (undugu wa damu) kama alivyo sema Mwenyezi Mungu mtukufu: (Na kila mmoja tumemwekea warithi katika waliyo yaacha wazazi wawili na jamaa. Na mlio fungamana nao ahadi wapeni fungu lao..), alipo maliza kuunga undugu baina ya Muhajirina na Answari wote, Amirulmu-uminina Ali (a.s) akaja kwa mtume (s.a.w.w) huku macho yake yanalenga lenga machozi akasema: (Ewe mtume wa Mwenyezi Mungu, umeunga undugu baina ya maswahaba wako wote, na haujaunga udugu baina yangu na swahaba yeyote?) Mtume (s.a.w.w) akasema: (Ewe Ali.. hauridhiki kua wewe ni ndugu yangu?) akasema (a.s): (Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu nimeridhika). Ndipo akasema Mtume wa Mwenyezi Mungu (s.a.w.w): (Wewe ni ndugu yangu hapa duniani na akhera).

Kufatia kauli hiyo mshairi Abuu Tammam anasema:

Ndugu yake ukihesabu ufahari pia ni mkwe wake. Hakuna mwenye ndugu mfano wake wala mwenye mkwe kama yeye.

Tukio la kuunga undugu alilofanya Mtume (s.a.w.w) ni miongoni mwa jambo muhimu katika siasa zinazo himizwa na uislamu ndani ya Qur’an tukufu, Mwenyezi Mungu mtukufu anasema: (Hakika ya waumini ni ndugu), japokua hakija simuliwa ndani ya Qur’an tukufu kisa cha kuunga undugu baina ya Muhajirina na Answari, lau zisinge pokelewa hadithi sahihi na ushahidi wa kihistoria unao thibitisha tukio hili, tungesema hiki ni kisa cha kutunga, kwa sababu yaliyo jiri (tokea) kufuatia undugu huo hayaelezeki, hayakua ya kufikirika bali yaliingizwa katika matukio halisi ya maisha, maswahaba walijitolea vitu vingi sana kuwasaidia ndugu zao kwa kiasi haija wahi kutokea katika umma wowote ukarimu wa juu kiasi hicho, kuna haja kubwa ya kuliangalia tukio hili na kuchukua mafunzo na mazingatio ndani yake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: