Kisomo maalum cha Qur’an kinacho simamiwa na Maahadi ya Qur’an katika siku zote za mwezi mtukufu wa Ramadhani..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya Qur’an iliyo andaliwa na Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kuhuisha siku za mwezi mtukufu wa Ramadhani, ulitengwa muda kwa ajili ya kisomo cha vijana, ambao husoma Qur’an tartiil wakisimamiwa na kamati ya tah-fidh chini ya kituo cha kuandaa wasomi na mahafidh cha Maahadi, kisomo hiki kinaendeshwa ndani ya jengo la Alqamiy lililo chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu kwa kushiriki idadi kubwa ya wasomi wa Qur’an walio chaguliwa baada ya kufaulu mtihani wa Qur’an ulio tolewa na kamati maalum.

Kisomo hiki ni sehemu ya kufanyia kazi kauli ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Wa-adabisheni (wafundisheni) watoto wenu mambo matatu: kumpenda Mtume wenu, na kuwapenda watu wa nyumbani kwake, na kusoma Qur’an, hakika wasomaji wa Qur’an watakua katika kivuli cha Mwenyezi Mungu siku ambayo hakutakua na kivuli ispokua hicho), miongoni mwa mambo muhimu yaliyo pelekea Maahadi kuchakua kundi hili la vijana ni akwa ajili ya kuhakikisha wanapata malezi yenye misingi ya Qur’an na kuhakikisha wanatumia vizuri umri wao katika kipindi chote cha mwaka hasa mwezi wa Ramadhani mtukufu, hii itawasaidia katika maisha yao, kwani mtu anaye kua katika misingi ya Qur’an hua mtu makini na mwenye kujiamini, huishi bila hofu wala matatizo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu mtukufu, kwani atakua na majibu ya kila tatizo atakalo kutana nalo katika maisha yake.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba maalumu ndani ya mwezi wa Ramadhani, ya kusoma Qur’an tukufu au kufanya mashindano ya Qur’an na mengineyo, ndani ya jengo la Maahadi au katika matawi yake yaliyo enea katika mikoa mingi ya Iraq, kwa ajili ya kueneza tamaduni za Qur’an tukufu na kusaidia usomaji wa Qur’an yote katika kipindi hiki cha mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: