Miongoni mwa ratiba maalumu ya mwezi wa Ramadhani mtukufu, kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha cha Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya kinatoa mihadhara kuhusu maarifa ya Qur’an (Ulumul-Qur’an), ndani ya ukumbi mtukufu wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na watumishi wa Ataba tukufu na mazuwaru, mihadhara hiyo hutolewa siku mbili katika kila wiki.
Kiongozi wa kituo tajwa hapo juu, Shekh Dhiyaau Dini Aali-Majeed Zubaidiy aliuambia mtandao wa Alkafeel kua: “Mwezi wa Ramadhani ni msimu wa Qur’an kama ilivyo pokelewa katika riwaya za Ahlulbait (a.s), miongoni mwa riwaya hizo ni kauli ya imamu Baaqir (a.s) isemayo: (Kila kitu kina msimu wake na msimu wa Qur’an ni mwezi wa Ramadhani), hivyo Maahadi ya Qur’an na kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha, tunaendesha mihadhara kuhusu maarifa ya Qur’an tukufu, namna ilivyo teremshwa, kuandikwa, visomo vyake na hati zake pamoja na mambo mengine”.
Akaongeza kusema kua: “Tunapo soma Qur’an tunaona imeandikwa kwa hati ya Othmani au imeandikwa kwa mujibu wa riwaya ya Hafswa iliyo pokelewa na Aaswim, ambapo maandishi yake yanatofautiana na maandishi ya kawaida, kuna alama za wakfu na zinginezo, hali kadhalika kugawanyika Qur’an hii katika juzuu thelethini, nani aliye igawanya? Na nini maana ya Makiyya na Madaniyya? Na mengineyo mengi yanayo hitajia ufafanuzi ndani ya Qur’an tukufu, pia kuna nukta nyingine muhimu ambayo ni namna ya kuamiliana na Qur’an tukufu, je inafaa kuisoma kama vitabu vya kawaida? Au lazima isomwe kwa mazingatio? Tumeelezea mambo haya kama alivyo sema Amirulmu-uminina (a.s): (Hakuna heri katika kisomo kisicho kua na mazingatio) hivyo tunajaribu kufafanua vipengele hivyo katika mihadhara yetu”.
Kumbuka kua kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha huendesha semina nyingi kuhusu Qur’an, hasa maarifa ya Qur’an (Ulumul-Qur’an) pamaja na nadwa na mikutano mbalimbali inayo zungumzia Qur’an.