Atabatu Abbasiyya tukufu yajiandaa kuhuisha kumbukumbu ya kuzaliwa kwa imamu Hassan Almujtaba (a.s)..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu ya mwezi wa Ramadhani ni kumbukumbu ya kuzaliwa kwa Mkarimu wa Ahlulbait na bwana wa vijana wa peponi imamu Hassan Almujtaba (a.s) ambapo inasadifiana na siku ya kesho katikati ya mwezi wa heri na rehema, mwezi ambao amejinasibisha nao Mwenyezi Mungu mtukufu, imamu ambaye anatuangazia nuru miongoni mwa nuru za watu wa watano wa kisaa maasumina (a.s), kama kawaida ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika kuhuisha minasaba ya mazazi ya maimamu wa Ahlulbait (a.s), itafanya kumbukumbu ya kuzaliwa kwa imamu Hassan Almujtaba (a.s), ambaye kuzaliwa kwake kulileta furaha kubwa kwa Mtume (s.a.w.w), miongoni mwa mambo yatakayo fanywa na Ataba ya ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) ni:

  • 1- Kuweka mapambo yanayo ashiria furaha ndani na nje ya Atabata tukufu yatakayo ashiria tukio hili tukufu na kuwafanya mazuwari wahisi amani na furaha.
  • 2- Kuzipamba korido za Ataba kwa mabango yanayo elezea utukufu wa imamu Hassan (a.s).
  • 3- Kuweka mabango ya mwanga na nyeradi katika milango ya Ataba tukufu na sehemu zingine za haram tukufu.
  • 4- Kuendesha kongamano la mkarimu wa Ahlulbait (a.s) katika mji wa Hillah tarehe kumi na nne ya mwezi wa Ramadhani na litaendelea kwa muda wa siku tatu litakalo kua na vitu vingi.
  • 5- Kuendesha kongamano la kuzaliwa kwa imamu Hassan (a.s), litakalo fanywa na idara ya watoto na makuzi chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Ataba tukufu.
  • 6- Kufanya kipindi katika redio ya Alkafeel ya wanawake kwa ajili ya kuelezea mnasaba huu.
  • 7- Kutoa machapisho maalumu kuhusu mnasaba huu.
  • 8- Kujiandaa kwa ajili ya kupokea makundi ya watu watakao kuja kutoa mkono wa pongezi.

Pia kuna vitu vingine vitahusika ndani ya ratiba.

Kumbuka kua iamau Hassan Almujtaba mtoto wa Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s) alizaliwa mwaka wa tatu hijiriyya usiku wa Juma Nne , katikati ya mwezi wa Ramadhani mtukufu, Jibrilu akashuka kutoka mbinguni hadi kwa Mtume (s.a.w.w) akamuambia: Hakika Mwenyezi Mungu anakutolea salamu na anakuambia jina lake umwite Hassan, Mtume akafanya hivyo na akamchinjia hakika na kunyoa nywele zake kisha akatoa sadaka ya fedha kwa uzito wa nyele hizo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: