Katika kuwakumbuka walio jitolea nafsi zao kwa ajili ya kulinda nchi: kamati ya kusimamia mashindano ya Qur’an ya kusoma kwa vikundi ya kitaifa, yawapa zawadi watoto wa mashahidi wa Hashdi Sha’abi..

Maoni katika picha
Kutokana na utukufu wa mwezi wa Mwenyezi Mungu na kuwatambua mashahidi wetu walio itikia mwito wa Marjaa dini mkuu wa kuihami aridhi ya Iraq na maeneo matukufu, na kufuatia muelekeo wa Atabatu Abbasiyya wa kuthamini damu za mashahidi walio jitolea kila walicho nacho kwa ajili ya kuihami nchi hii, kamati ya kusimamia mashindano ya Qur’an ya kusoma kwa vikundi ya kitaifa awamu ya tatu yanayo endelea katika ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) imeingiza katika ratiba yake kipengele cha kutoa zawadi kwa mayatima ambao ni watoto wa mashahidi wa Hashdi Sha’abi, kama sehemu ya kutekeleza maagizo ya Marjaa dini mkuu ya kuwaenzi mashahidi wetu kwani wao ni watu watukufu zaidi.

Mkuu wa Maahadi ya Qur’an tukufu na msimamizi wa mashindano haya aliye simamia utoaji wa zawadi hizo Shekh Jawaad Naswirawiy alisema kua: “Katika mwezi huu mtukufu wa Ramadhani tunaishi katika mazingira bora ya kiroho ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), utukufu wa mazingira haya baada ya Mwenyezi Mungu unarejea katika damu zilizo mwagika kwa ajili ya kulinda aridhi hii, na kuleta amani na utulivu kwa wairaq pamoja na kusafisha miji ya Iraq kutokana na uchafu wa matakfiri ya Daesh”.

Akaongeza kusema kua: “Tumeingiza ratiba hii kama sehemu ya msisitizo kua mashahidi na watoto wao wamekaa katika akili zetu, jambo hili linalo fanywa na Atabatu Abbasiyya kupitia Maahadi ya Qur’an ni kuwaonyesha walio poteza wasaidizi wao katika uwanja wa vita kua wapo wanao wajali, hakika tunacho kitoa kwa watoto wa mashahidi ni kitu duni sana ukilinganisha na namna baba zaoa walivyo jitolea”.

Tunakumbusha kua zawadi hizi hutolewa kila siku mwishoni mwa ratiba ya mashindano, zawadi hizo hukabidhiwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) na wajumbe wa kamati kuu ya uongozi pamoja na marais wa vitengo hali kadhalika wajumbe wa kamati inayo simamia mashindano haya.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: