Atbatu Abbasiyya tukufu yamkumbuka Allaama Shekh Ali Samaka Alhilliy (q.s)..

Maoni katika picha
Atabatu Abbasiyya kupitia kituo cha turathi za Hilla chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu kimemkumbuka mmoja wa watu muhimu katika mji wa Hilla ambaye ni Allaama Shekh Ali Samaka Alhilliy (q.s), ambaye alikua na athari kubwa katika mji huu ulio julikana toka zamani kama mji unaozaa maulamaa na watu watukufu, kwa zaidi ya karne tatu ulikua ni kimbilio la watafuta elimu na maarifa ya kibinadamu, katika mji huu walihitimu wanazuoni wengi sana wasio kua na idadi.

Hayo yalisemwa katika hafla iliyo fanyika jana Ijumaa (13 Ramadhani 1438h) sawa na (09 Juni 2017m) katika bustani za mazaru ya Radu Shamsi ndani ya mji wa Hilla makao makuu ya mkoa wa Baabil, pembezoni mwa kongamano la mkarimu wa Ahlulbait (a.s) linalo fanywa na Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya), litakalo anza rasmi jioni ya Juma Mosi kwa ajili ya kuhuisha kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbait imamu Hassan (a.s).

Hafla ilihusisha kisomo cha aya tukufu ndani ya kitabu kitakatifu, kisha ukasomwa ujumbe wa kamati inayo simamia mradi wa (Hilla ni mji wa imamu Hassan –a.s-), na ujumbe wa kituo cha turathi za Hilla ulio wasilishwa na Shekh Swadiq Khawilidiy mkuu wa kituo, kisha ukafuata ujumbe wa familia ya Samaka, halafu ikaonyeshwa filamu iliyo andaliwa na kituo cha turathi za Hilla inayo elezea uhai wa Aalimu huyu mkubwa.

Kumbuka kua Allaama Shekh Ali Samaka Alhilliy (q.s) alizawa mwaka wa (1901m) katika mji wa Hilla, alijifunza kusoma na kuandika kwa baba yake, toka utoto wake alikua anapenda elimu na mwepesi wa kujifunza na kuhifadhi, kutokana na kupenda kwake elimu alienda katika mji wa Najafu na akasoma kwa mashekhe wakubwa huko kama vile Sayyid Said Alhakeem na Sayyid Abuu Qassim Alkhui na Sayyid Muhsin Alhakeem hadi akafikia kiwango cha Ijtihadi, akawa mwalimu katika hauza ya Najafu katika kitivo (mchepuo) wa Fighi, miongoni mwa wanafunzi wake ni dokta Shekh Ahmad Waailiy kiongozi wa mimbari ya imamu Hussein (a.s) na wanazuoni wengine wengi, ameandika vitabu vingi, cha mwisho ni (Qabsu min Tafsirul Qur’an Alkareem) amefariki mwaka wa (1970m) watu wa Hilla wazee kwa vijana walitoka kusindikiza jeneza lake.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: