Kufuatia kumbukumbu tukufu ya kuzaliwa kwa mkarimu wa Ahlulbait imamu Hassan (a.s) jioni ya siku ya Ijumaa (13 Ramadhani 1438h) sawa na (09 Juny 2017m) yalihitimishwa rasmi mashindano ya Qur’an awamu ya tatu yaliyo endeshwa na kituo cha kuandaa wasomi na mahafidh katika Maahad ya Qur’an tukufu chini ya Atabatu Abbasiyya, katika ukumbi wa haram tukufu ya Abulfadhil Abbasiy (a.s) kwa kushiriki vikundi (24) kutoka mikoa yote ya Iraq.
Hafla hiyo ilihudhiriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhamma Ashiqar (d.t) pamoja na jopo la wajumbe wa kamati kuu ya uongozi na marais wa vitengo, pamoja na mazuwaru, kikosi cha Dhiqaar kilipata nafasi ya kwanza na kiliwasilishwa na (Msomaji Is-haqa Kaadhim, Hafidh Abdul-adhim Abdulhussein na mfasiri Ustadh Muhammad Kaamil), kilikipiku kikosi cha Karbala kilicho wasilishwa na (Msomaji Abdallah Hussein, Hafidh Mustwafa Sa’adun na Mfasiri Ustadh Hamza Daakhil).
Kumbuka kua mashindano haya ya Qur’an yalianza toka siku ya kwanza ya mwezi mtukufu wa Ramadhani, yalikua yanarushwa na chanel (tv) ya Furaat, yamefanyika kwa mujibu wa ratiba maalumu ya Maahadi ya Qur’an katika mwezi wa Ramadhani, ambapo yameshirikisha mikoa mbalimbali ya hapa Iraq, mashindano haya yalihusisha hukumu za Qur’an, hifdhu na tafsiri.