Ujumbe wa umoja wa mataifa nchini Iraq: Kikosi cha Abbasi cha wapiganaji kinatoa huduma nyingi za kibinadamu zinazo endana na mchango wao kijeshi katika kukomboa miji ya Iraq iliyo tekwa na magaidi..

Maoni katika picha
Kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kimetangaza kupokea ugeni kutoka umoja wa mataifa katika ofisi zake zilizopo mkoani Karbala, kikao cha kuzungumza na wageni hao kilihudhuriwa na kiongozi mkuu wa kikosi cha wapiganaji Shekh Haitham Zubaidiy, walijadiliana baadhi ya mambo muhimu kuhusu vita inayo endeshwa na jeshi la serikali wakishirikiana na Hashdi Sha’abi kwa ajili ya kukomboa aridhi zilizo tekwa na magaidi ya Daesh, pamoja na kuzingatia huduma za kibinadamu zinazo tolewa kwa raia na wakimbizi kwa ujumla, wakati huohuo wakatoa wito wa kuongeza juhudi.

Kikosi hicho kimebainisha kua: ugeni ulimuambia kiongozi mkuu wa kikosi cha Abbasi (a.s) cha wapiganaji kua, wamechagua kufanya mazungumzo na kikosi hiki kwa sababu wameona pamoja na kushiriki kwao kijeshi; bado wanatoa msaada mkubwa wa huduma za kibinadamu kwa ajili ya kukomboa miji ya Iraq iliyo tekwa na magaidi, hilo ndio jambo kubwa lililo wasukuma kuja Karbala na kukutana na viongozi wa kikosi hiki, huu ni mwanzo muhimu na una matokea chanya kutokana na nafasi ya umoja wa mataifa katika kutoa misaada ya kimataifa na watakua na athari nzuri kwa vyombo vya wapiganaji wa Hashdi Sha’abi.

Nanye kiongozi mkuu wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) alielezea huduma za kibinadamu zinazo tolewa na ofisi ya Muheshimiwa Sayyid Ali Sistani (d.dh.w), akasisitiza kua huduma hizo zinashinda huduma zinazo tolewa na umoja wa mataifa ambao unapata misaada ya kimataifa, akabainisha kua: ugeni umeahidi kuongeza juhudi katika kutoa huduma za kibinadamu kwenye miji tofauti, pia wakamuomba kiongozi wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) kutembelea ofisi zao zilizopo katika mji mkuu wa Bagdad.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: