Kuainisha siku za Lailatul Qadri kwa mujibu wa Sayyid Sistani (d.dh.w)..

Maoni katika picha
Tukiwa tunakaribia siku tukufu za Lailatul Qadri maswali yamekua mengi kuhusu kuainishwa kwa siku hizo, ofisi ya Sayyid Sistani (d.dh) imeonyesha jawabu la swali lililo ulizwa kuhusu swala hili.

Swali linasema:

Muheshimiwa Sayyid (d.dh) anamtazamo gani kuhusu kuainisha siku za Lailatul Qadri? Na ni yapi matarajio yenye nguvu kwake kuhusu swala hili… kutoka kwa jopo la waumini.

Jibu:

Kwa jina la Mwenyezi Mungu mtukufu, matarajio makubwa itakua moja ya siku mbili (mwezi ishirini na moja na mwezi ishirini na tatu), inawezekana pia ukawa ni usiku wa mwezi kumi na tisa, yawapasa waumini kufanya ibada maalumu katika usiku wa siku tatu hizo, tunakuombeni dua..
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: