Tangazo la washindi wa shindano la kitafiti la wanahabari wakike..

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya shindano la kitafiti la wanahabari wa kike lililo endeshwa katika kongamano la kwanza la wanahabari hao na kusimamiwa na jarida la Riyadhu Zaharaa (a.s) chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, imetangaza majina ya watu walioshinda katika shindano hilo, ambalo walishiriki wanahabari wa kike bamoja na waandishi wa majarida wa kike pia, matokea ya washiriki yalikua kama yafuatavyo:

  • 1- Khadija Hassan Ali Alqaswir kutoka Najafu Ashrafu katika utafiti wake kuhusu (Umuhimu wa uthibitisho wa wanahabari na nafasi yao katika kutunza historia isipotoshwe).
  • 2- Hanaau Baaqir Kamaru Alkhafaji kutoka mkoa wa Dhiqaar katika utafiti wake kuhusu (Mtazamo wa wanahabari kuhusu kutangaza maswala ya wanawake).
  • 3- Rasha Abduljabaar Naasir kutoka mkoa wa Basra katika utafiti wake kuhusu (Kuwepo wanahabari waislamu wenye maadili).

Kamati iliandaa pia zawadi kwa washiriki waliobaki wa shindano hili.

Kumbuka kua shindano lilikua linalenga mambo yafuatayo:

  • 1- Kuangalia changamoto wanazo kutana nazo wanahabari wa kike wenye maadili mema.
  • 2- Namna ya kunufaika na uelewa wa wanahabari.
  • 3- Kutengeneza uhusiano wa wanahabari unao rahisisha utekelezaji wa majukumu ya wanahabari wenye maadili mema.
  • 4- Namna ya kupambana na vyombo vya habari viovu.
  • 5- Umuhimu wa kusoma fani za namna ya kutoa majibu.
  • 6- Nafasi ya vyombo vya habari katika kurekebisha umma na kutunza historia.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: