Kufatia utukufu wa mwezi wa Ramadhani kamati ya kusaidia chini ya Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani (d.dh.w) inaendelea kutoa misaada ya lazima kwa wakimbizi kama ratiba ilivyo pangwa, pamoja na mazingira ya hali ya joto na swaumu walizo nazo, mazingira magumu ya hali ya hewa yamekua ni kichocheo cha kuwafanya waongeze juhudi katika kusaidia familia zilizo kimbia mateso ya magaidi ya Daesh, program hii ni miongoni mwa misaada ya kibinadamu, tunasaidia wakimbizi wakubwa kwa watoto ili kuwajengea furaha na kuwafanya waishi maisha ya kawaida wakati wakisubiri kukombolewa kwa miji yao, kwani wapo katika maeneo mabaya sana, maeneo ambayo hayana vitu muhimu katika maisha ya mwanadamu, tumegawa misaada ya kibinadamu katika kitongoji cha Huweija na kijiji cha Shahama pembezoni ya mji wa Tikriti, hali kadhalika tulipeleka misaada kwa baadhi ya familia zenye mahitaji maalumu, wajane na mayatima.
Familia za wakimbizi zilishukuru sana undugu na upendo wa hali ya juu walio onyeshwa na watu walio wapelekea misaada chini ya ofisi ya Marjaa dini mkuu, wakawapa salamu za dhati wamfikishie Marjaa dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Sistani (d.dh).
Kumbuka kua Marjaa dini mkuu amewaomba wananchi kutitia Hotuba za Ijumaa, kutoa misaada ya kibinadamu kadri ya uwezo wao, ambapo alisema kua: “Kutokana na kuongezeka kwa wakimbizi katika maeneo yenye vita, na kukosekana kwa mahitaji muhimu ya kibinadamu kwao, tunawaomba wananchi watukufu kutoka kila mkoa wajitolee kadri ya uwezo wao kuwasaidia ndugu zao kwa kuwapa mahitaji muhimu ya kibinadamu ili kuwapunguzia machungu wanayo pitia, hakika mambo bora zaidi wanayo takiwa kufanyiana watu wa nchi moja ni kusaidiana wakati wa matatizo”.