Kwa picha: Mahudhurio ya wasoma Qur’an Tartiil katika haram ya Abbasi (a.s)..

Maoni katika picha
(Katika nyumba alizo ruhusu Mwenyezi Mungu ziinuliwe na kutajwa ndani yake jina jake) vyasikika visomo vizuri vya Tartiil ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mwezi mtukufu wa Mwenyezi Mungu, mwezi ambao waumini wapo katika ugeni wake, vikao vya kusoma Qur’an vinaendelea kila siku, hakika Qur’an ni pambo la nyoyo na msimu wake ni katika mwezi mtukufu wa Ramadhani, kufuatia kauli tukufu ya Mtume (s.a.w.w) isemayo: (Atakaye soma aya moja ndani ya mwezi wa Ramadhani ataandikiwa thawabu sawa na aliye soma Qur’an nzima katika miezi mingine), hivyo utawaona waumini wakijihimiza kusoma Qur’an katika eneo hili tukufu ndani ya mwezi mtukufu, kwa kushiriki visomo hivi kila siku, mtu anaweza kujifundisha kusoma kwa usahihi pamoja na hukumu za Tajwid.

Kumbuka kua Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya imeandaa ratiba na utaratibu maalumu wa kuhuisha siku hizi tukufu kwa kuendesha visomo vya Qur’an, mashindano ya Qur’an na mengineyo, ndani ya Maahadi au katika matawi yake yaliyopo katika mikoa mingi ya Iraq, kwa ajili ya kueneza utamaduni wa kusoma Qur’an katika mwezi wa Ramadhani, na kuwasaidia watu waweze kusoma Qur’an nzima katika mwezi huu mtukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: