Hakika ni siku ya kwanza katika siku za Laitatul Qadri tukufu, usiku wa kumi na tisa wa mwezi wa Ramadhani, siku aliyo jeruhiwa kiongozi wetu Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s), kundi kubwa la waumini kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala wamekuja kuhuisha msiba huu, waombolezaji wamejaa katika haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), wenye kusimama, kukaa, kurukuu, kusujudu huku sauti kama za kundi ya nyuki zikisikika, wenginye wanasoma dua, huku wengine wakisoma Qur’an na wengine wanasoma tasbihi na istighfaar.
Mazuwaru wanafanya ibada zao kwa kusoma dua, kuswali tahajudi, kusoma Qur’an, na adhkaari maalumu za usiku huu, kwa ajili ya kutafuta msamaha na kuepukana na moto, pia wanakumbuka tukio la kujeruhiwa kwa Amirulmu-uminina Ali (a.s) katika usiku kama wa leo akiwa miharabuni anaswali swala ya Alfajiri, yote hayo yanafanyika chini ya uangalizi makini wa watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s), ambao wamejipanga vizuri kutoa huduma bora katika usiku huu na siku zingine zote ndani ya haram tukufu au nje, watu waliendelea kufanya ibada hadi asubuhi.
Kumbuka kua usiku wa kumi na tisa wa mwezi wa Ramadhani unatarajiwa kua ndio usiku wa kwanza wa siku za Lailatul Qadri, ambazo ubora wake haufikiwi na siku yeyote ile, kufanya ibada katika siku hiyo ni bora kuliko kufanya ibada miezi elfu moja, katika usiku huo hukadiriwa mambo ya mwaka mzima, huteremka malaika pamoja na Jibrilu (a.s) kwa idhini ya Mwenyezi Mungu, huenda kwa Imamu wa zama (a.s) na kumuonyesha mambo yaliyo kadiriwa kwa kila mtu.