Ilidaiwa kufanyika hukumu ya kunyanyua misahafu isiyo ongea badala ya kunyanyua msahafu unao ongea –Imamu Ali (a.s)-, likachupa mipaka kundi la Khawaariji, likatoka kupigana na imamu wa zama zao Ali (a.s), imamu Ali (a.s) aliwanasihi na kuwapa mawaidha lakini waliendeleza uadui wao (walipambiwa na shetani wakasahau utajo wa Mwenyezi Mungu…), wakaunda jeshi na wakahalalisha damu ya Amirulmu-uminina (a.s) na damu ya watu wote walio chini ya bendera yake.
Wakajiandaa kupigana na jeshi la imamu (a.s), ikalazimika imamu apigane nao hadi alipo washinda katika vita vya Nahrawan.
Baada ya vita hiyo kundi la Makhawaariji walio shindwa katika uwanja wa vita wakafanya kikao katika mji mtukufu wa Maka, kwa kuwasiliana na kushauriana na Muawiya bun Abuu Sufiyan, ambaye alimteua mmoja wao Abdurahman bun Muljim Almuraadi, wakashauriana na kumuandaa bun Muljim kwa zana mbalimbali (ili aende kumuua imamu Ali –a.s-) pia kutokana na chuki aliyo kua nayo kwa Ahlulbait (a.s). walimuandalia siraha na wakampa mbinu za mashambulizi pamoja na kumteulia mtu atakae msimamia, ilipo fika Alfajiri ya tarehe kumi na tisa mwezi wa Ramadhani mwaka wa (40h), ibun Muljim alimvizia Amirilmu-uminina Ali (a.s) na kumpiga upanga kichwani kwake wakati akiswali sunna ya Alfajiri ndani ya msikiti mtukufu wa Kufa, kipindi ambacho umma wa kiislamu ulikua unakaribia kupata ushindi dhidi ya matwaghuti katika vita na Muawiya huko Sham.
Amirulmu-uminina Ali (a.s) alipata maumivu makali sana kutokana na jeraha hilo baya alilo katwa na upanga uliotiwa sumu, aliugulia jeraha lake usiku na mchana kwa muda wa siku tatu, malaika mbinguni wakamuombea dua na kikavuma kimbunga cha upepo mweusi, Jibril (a.s) akanadi baina ya mbingu na aridhi kwa sauti iliyo sikiwa na kila aliye macho. “Wallahi zimevunjika nguzo za uongofu.. wallahi zimezimika nyota za mbinguni na bendera ya uchamungu imeanguka.. ameuawa mtoto wa Ammi wa Muhammad Almustwafa.. ameuawa Wasii mteule.. ameuawa Ali mridhiwa.. wallahi ameuawa mbora wa mawasii.. ameuliwa na muovu wa waovu”.
Amirulmu-uminina Ali (a.s) kutokana na maelekezo ya Mtume (s.a.w.w) alikua amesha mteua mwanae Hassan (a.s) kushika uongozi baada yake, siku tatu za machungu kwa imamu Ali (a.s) ziliisha akimtaja Mwenyezi Mungu na kusema nimeridhia hukumu yake na ninajisalimisha katika hekima yake.
Alikua anawahusia wanae pamoja na watu wengine na kuwataka wasimamishe hukumu ya Mwenyezi Mungu mtukufu, akiwatahadharisha kuharibiwa ujumbe wa kiislamu, na kuto rejea nyuma katika kunusuru uislamu, na hii ni sehemu ya wasia wake:
“Kuweni maadui wa wenye kudhulumu na wasaidizi wa wenye kudhulumiwa, nakuusieni pamoja na watoto wangu wote na kila atakae fikiwa na ujumbe wangu huu, kumcha Mwenyezi Mungu na kupangilia mambo yenu na kusuluhisha (migogoro) baina yenu,.. Allah allah (wajalini) mayatima.. Allah allah majirani zenu.. Allah allah Qur’an.. Allah allah nyumba ya Mola wenu msiitelekeze kwa muda wote mtakao kua hai.. Allah allah jihadi kwa mali zenu, nasfi zenu na ndimi zenu (zitumieni) katika njia ya Mwenyezi Mungu.. shikamaneni na kuwasiliana na kusaidiana, jihadharini na kutowasiliana na kutengana, msiache kuamrisha mema na kukataza mabaya (mkiacha hayo) mtatawaliwa na watu waovu kisha mtakua mnaomba na hamjibiwi.. Tambua; iwapo nikifa kutokana na pigo hili mlipize kisasi kwa kumpiga pigo moja, wala msisulubu mwili wake, hakika nilimsikia Mtume (s.a.w.w) anasema (Jiepusheni na kusulubu maiti hata kama ni ya mbwa kichaa).
Amami iwe kwake mwanaume mwenye haki na uadilifu siku aliyo zaliwa ndani ya Kaaba na siku aliyo uawa kishahidi akiwa katika sijda ndani ya mihrabu na siku atakayo fufuliwa hai akinyesheleza watu katika hodhi.