Miongoni mwa ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya mwezi wa Ramadhani kuna kipengele cha kuhuisha tukio hili lenye kuumiza litakalo enda sambamba na kuhuisha siku ya Lailatul Qadri ya kwanza, miongoni mwa vipengele vya ratiba hiyo ni:
- 1- Kuweka mapambo meusi yanayo ashiria huzuni kutokana na tukio hili katika maeneo yeto ya Atabatu Abbasiyya tukufu pamoja na kufunga taa zenye mwanga mwekundu.
- 2- Kuelekeza mwanga katika maeneo yanayo tolewa mihadhara ya kila siku ndani ya haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) hasa inayo husu msiba huu, na itaendelea hadi mwezi ishirini na moja ambayo ndio siku alikufa kishahidi.
- 3- Kufanya majlis ya kuomboleza katika ukumbi wa utawala wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ambapo yatatolewa mawaidha na kuibwa qaswida za maombolezo.
- 4- Siku ya kufariki imamu Ali (a.s) watumishi watatoka katika maukibu (kundi) moja na kwenda hadi katika haram ya Imamu Hussein (a.s) kwa ajili ya kwenda kuhani na kufanya majilisi ya maombolezo katika haram hiyo tukufu.
- 5- Kujiandaa kupokea misafara ya waombolezaji katika malalo ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).
- 6- Kujiandaa kupokea watu watakao kuja kutoa pole na kuwawekea mazingira mazuri yatakayo wawezesha kufanya ibada zao kwa amani na utulivu katika siku hizi za kuhuisha Lailatul Qadri.
Hii ni sehemu inayo husu tukio la taazia tu, huku ratiba ya Atabatu Abbasiyya tukufu ya mwezi wa Ramadhani iliyo anza kutekele