Maelezo kuhusu walio jiandikisha katika sehemu ya ziara kwa niaba..

Maoni katika picha
Mtandao wa kimataifa Alkafeel umetoa ufafanuzi kuhusu wanao jiandikisha katika sehemu ya ziara kwaniaba, ambayo ni moja ya sehemu za mtandao huo, kua wamefungua mlango wa kujiandikisha kwa ajili ya zira kwa niaba, inayo husisha kumzuru imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kila siku pamoja na siku za Ijumaa, zote hizo ni ziara maalum, ikiwemo na ziara ya imamu Hassan (a.s) ndani ya mji wa Madina (Baqii Gharqad) katika kukumbuka kuzaliwa kwake, ili kuendelea kumzuru imamu Hussein (a.s) katika ziara maalum ndani ya siku za Lailatul Qadri tukufu pamoja na usiku wa Iddi na mchana wake.

Idara ya mtandao wa Alkafeel imependelea kuacha mlango wazi kwa ajili ya kuendelea kupokea maombi ya ziara kwa niaba ndani ya mwezi wote wa Ramadhani, yatafanyiwa kazi baada ya Iddi Fitri tukufu inshallah. Tambua kua ziara zote zinatekelezwa pamoja na swala, dua, kama ilivyo pangwa kwa kila ziara, hivyo mtandao wa Alkafeel unamjulisha kila aliye jiandikisha kua ziara yake imesha fanywa hata kama ikichelewa kuonyeshwa katika jeduali la majina.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: