Watumishi wa Atabatu Abbasiyya tukufu waendelea na maombolezo ya kuuawa kishahidi kwa Amirulmu-uminina Ali (a.s)..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba ya maomboleza katika Atabatu Abbasiyya tukufu, kumbukumbu ya kuuawa kishahidi kwa Amirulmu-umina Ali bun Abuutwalib (a.s) kufuatia kauli ya imamu Jafari Swadiq (a.s) isemayo: (Huisheni mambo yetu, Mwenyezi Mungu atamrehemu atakaye huisha mambo yetu), kwa ajili ya kuhuisha huzuni na maombolezo watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wamefanya kumbukumbu ya msiba huu ulio tokea katika umma wa kiislamu ndani ya siku kama hizi mwaka wa (40) hijiriyya kwa kuanguka nguzo ya tatu ya uongofu baada ya kuanguka nguzo mbili ambazo ni Mtume mtukufu na binti yake Zaharaa (a.s), kumbukumbu hiyo imefanywa ndani ya ukumbi wa imamu Hassan (a.s) katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kuhudhuriwa na kundi kubwa la watumishi.

Baada ya Qur’an tukufu na surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashahidi wa Iraq walio uawa kwa ajili ya kulinda nchi hii na ambao wamejifunza ushujaa kutoka kwa huyu tunae mkumbuka, kulikua na muhadhara wa Shekh Ali Muhani kutoka katika kitengo cha dini cha Ataba tukufu, baada ya kutoa mkono wa pole kwa wahudhuriaji na umma wa kiislamu kwa ujumla alizungumzia mas-ala ya kuwajibikiwa kwa jumla na kuwajibikiwa maalum (Takliful aamu wa takliful khaasu), na namna alivyo wajibika Mtume kumlea na kumtunza Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s) kabla ya kushuka wahyi na kufikisha ujumbe wa uislamu, Mtume (s.a.w.w) alimuandaa Ali kuupokea uislamu ili awe mtu wa mfano katika dini tukufu, anasema (a.s): (Mtume wa Mwenyezi Mungu alikua anatafuna chakula halafu ananilisha, kila sehemu aliyo enda nilikua pamoja naye), kama alivyo husia uongozi (ukhalifa) wa Ali bun Abuutwalib (a.s) ambapo aliendelea kua kiongozi hadi alipo uawa kishahidi na muovu wa waovu (maluun) Abdurahman bun Muljim.

Baada yake ikaonyeshwa filamu ya kihistoria (Mkubwa wa maswahaba), ambayo imetengenezwa na idara ya uzalishaji ya Alkafeel, ambayo inaangazia historia ya uhai wa Abuutwalib (r.a) mzazi wa Amirulmu-uminina (a.s).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: