Kwa kunyanyua mikono: Waumini wanahuisha usiku wa pili wa Lailatul Qadri na kukumbuka kuuawa kishahidi kwa Amirulmu-uminina (a.s)..

Maoni katika picha
Pembezoni mwa sehemu tukufu ya malalo ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) waumini wanahuisha usiku wa pili wa Lailatul Qadri kwa kuswali, kusoma Qur’an na kuomba dua. Usiku huu; una utukufu mkubwa kushinda usiku wa mwezi kumi na tisa, nao ni usiku wa mwezi ishirini na moja ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani. Katika siku hizi tukufu, Mwenyezi Mungu anatwita kutufungulia mlango wa toba na matarajio ya kukubaliwa kutokana na upole wake na ukarimu wake, tunatarajia shifaa (msamaha) wake tukiwa tumebeba vitendo vyetu mikononi mwetu, wakati huo huo waumini walikumbuka msiba unao umiza umma wa kiislamu wa kuuawa kishahidi kwa Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s), iliandaliwa sehemu maalumu ya maombolezo ambapo palitolewa muhadhara na zikaimbwa qaswida za maombolezo na Ali Basha.

Nao watumishi wa Ataba mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) tukufu wamejipanga kutoa huduma bora kwa mazuwaru, ili kuwawezesha kufanya ibada kwa utulivu na wepesi.

Kumbuka kua miongoni mwa kauli bora zilizo pokewa kuhusu kuhuisha Lailatul Qadri ni ile ya imamu Muhammad Baaqir isemayo: (Atakae huisha Lailatul Qadri atasamehewa dhambi zake, hata kama zitakua nyingi kama nyota za mbinguni au uzito wa milima au ujazo wa bahari), na umeitwa usiku wa Lailatul Qadri kutokana na ukubwa wa hadhi yake, katika usiku huo hupangwa vitendo vya waja vya mwaka huo na hupambanuliwa kila jambo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: