Tukio liumizalo nyoyo za wapenzi wa Ahlulbait (a.s) na wafuasi wao mashariki na magharibi ya aridhi, tukio hili linahuisha huzuni za watu wa nyumba ya mtume (s.a.w.w), Atabatu Abbasiyya hufanya majlis kila mwaka kwa muda wa siku nne mfululizo ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) kwa ajili ya kukumbuka kuuawa kishahidi kwa Amirulmu-uminina Ali bun Abuutwalib (a.s), ambapo hua ni miongoni mwa ratiba za maombolezo zilizoandaliwa na Atabatu Abbasiyya kwa ajili ya kuhuisha siku hizi zenye machungu makubwa.
Majlis hufanywa kila siku jioni kuanzia siku ya kujeruhiwa kwake; usiku wa mwezi kumi na tisa Ramadhani na huendelea hadi mwezi ishirini na mbili, huanza kwa kusomwa Qur’an tukufu kisha hufuatia muhadhara wa kidini kutoka kwa shekh Abdu Twaaiy, ambaye mihadhara yake ipo kila siku za mwezi huu mtukufu, lakini katika siku hizi za huzuni hujikita katika kuelezea msiba huu na mambo yanayo husiana na imamu Ali (a.s) kama vile historia yake na sifa zake tukufu ambazo ni nyingi mmno.
Baaba ya muhadhara hufuatia maatam na qaswida za maombolezo ambazo huibwa na Ali Basha Karbalai kwa ajili ya kuamsha hisia za huzuni na majonzi katika nafsi za wahudhuriaji, kutokana na tukio hili linalo umiza waislamu wote.