Kuendelea kwa mazungumzo ya ushirikiano baina yao Atabatu Abbasiyya tukufu na wizara ya afya ya Belarusia, wamesaini mkataba wa kusaidiana na kushirikiana baina yao, kwa ajili ya kubadilishana uzoefu na kunufaika kutokana na teknelojia na utaalamu wa kimataifa pamoja na kuangalia matumizi sahihi ya teknelojia yatakayo nufaisha pande zote mbili, yamefanyika haya kufatia ugeni wa wizara ya afya ya Belarusia ulio tembelea Atabatu Abbasiyya tukufu ukiongozwa na waziri wake bwana Valery Malashko.
Katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) alihudhuria utiaji saini huo pamoja na rais wa miradi ya kihandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh na mkuu wa hospitali ya Alkafeel dokta Haidari Bahadeli pamoja na jopo la wahandisi na wataalamu wa Ataba tukufu, kazi ya kwanza itakua kufunga na kuendesha kifaa cha uchunguzi wa vimelea cha Atabatu Abbasiyya tukufu, Muhandisi Dhiyaau Swaaigh aliuelezea ugeni kuhusu mradi huo na kiwango kilicho kamilika.
Waziri wa afya wa Belarusia alisema kua: “Tuna furaha sana katika ziara hii ambayo ni muendelezo wa mawasiliano ya nyuma baina ya Jamhuri ya Belarusia na Atabatu Abbasiyya tukufu, ugeni wetu una jopo la madaktari na wataalamu walio bobea katika kutengeneza dawa na vifaa vya uchunguzi wa vimelea, na hilo ndio jambo la kwanza tulilo kubaliana na kutiliana saini siku za nyuma”.
Muhandisi Dhiyaau Majidi Swaaigh aliongeza kusema kua: “Kufuatia makubaliano yaliyo fikiwa baina ya Atabatu Abbasiyya na wizara ya afya ya Belarusia mwezi ulio pita, sasa hivi sehemu ya makubaliano haya imeanza kutekelezwa, tumepokea mashirika ya Belarusia kwa ajili ya utekelezaji ya miradi ya Atabatu Abbasiyya tukufu, miongoni mwa miradi hiyo ni mradi wa ufungaji wa kifaa cha uchunguzi wa vimelea ambao shirika la Belarusia linasimamia kuufunga na kuuendesha, Atabatu Abbasiyya imekamilisha mradi huo asilimia sabini (%70) hadi sasa”,