Kwa kusaidiana na Atabatu Abbasiyya tukufu: Taasisi ya Biru Rahiim imefuturisha na kufanya kongamano la kuzizawadia familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba zake za mwezi wa Ramadhani na kwa kusaidiana na Atabatu Abbasiyya tukufu kupitia chuo cha masomo ya kibinadamu, taasisi ya Biru Rahiim ya kutoa misaada ya kimaendeleo tawi la Najafu wamefuturisha familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi pamoja na kufanya kongamano lililokua na vitu vingi, miongoni mwa vitu vilivyo fanyika katika kongamano hilo ni kutoa zawadi kwa mayatima walio faulu mitihani ya shuleni kwao, kwa ajili ya kuonyesha thamani ya kujitahidi kwao katika masomo na kuwashajihisha wao pamoja na wengine kuongeza juhudi zaidi katika miaka ijayo, pia kulikua na mashindano na maswali kuhusu Qur’an na walipewa zawadi walio shinda na kujibu vizuri, pia kulikua na usomaji wa mashairi na kaswida, vilevile zilitolewa zawadi kwa mayatima wote walipewa nguo na kapu la nafaka za chakula kwa ajili ya familia zao, kongamano lilihitimishwa kwa ujumbe uliotolewa na rais wa taasisi hiyo, dokta Muhammad Siraji, aliziahidi familia za mayatima kua wataendelea kuwasaidia na kuwajali kutokana na namna wazazi wao walivyo jitolea kwa ajili ya kuilinda Iraq na watu wake, kwa kiwango ambacho wasamalia wema watakavyo jitolea kwani hawapati msaada wowote kutoka serikalini, na akamaliza kwa kutoa shukrani za dhati kwa kila aliye changia katika kuzisaidia familia za mashahidi wa Hashdi Sha’abi.

Mkuu wa chuo cha masomo ya kibinadamu Ustadh Swafaau Abduljabaar Ali Mussawiy alisema kua: “Hakika haya tunayo fanya ndani ya mwezi wa Ramadhani ni mambo endelevu katika Atabatu Abbasiyya na taasisi ya Biru Rahiim katika kuwasaidia wapiganaji wa serikali na Hashdi Sha’abi bamoja na familia za mashahidi walio jitolea kila walicho nacho kwa ajili ya kuilinda nchi na dini”.

Ustadh Muhammad Siraji mkuu wa taasisi ya Biru Rahiim aliongeza kusema kua: “Kufuturisha pamoja na ratiba yetu ya mwezi wa Ramadhani ipo chini ya ulezi wa Muheshimiwa Sayyid Ahmad Swafi (d.i) kiongozi mkuu wa kisheria katika Atabatu Abbasiyya tukufu na kwa kushirikiana na mkuu wa chuo cha masomo ya kibinadamu, taasisi hii ilipo anzishwa mwaka (2016) ilikua inalea familia za mashahidi (80) na sasa hivi tuna zaidi ya familia (732), taasisi inaendelea kupanua wigo katika mikoa mingine pia, katika kipindi ambacho wapiganaji wetu wanapata ushindi mkubwa huko Musol, tunasisitiza kua hatutawasahau mashahidi zetu na familia zao tukufu katu”.

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu katika ratiba yake ya mwezi wa Ramadhani imeweka kipengele maalum cha kuwasiliana na familia pamoja na mayatima wa mashahidi wa Hashdi Sha’abi, sawa iwe katika kufuturisha au kuwapa vyakula na wakati mwingine huwapa msaada wa kipesa na mengineyo.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: