Uingiapo mwezi wa Ramadhani usiku na mchana utawaona watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) wakishindana katika kuwatumikia mazuwaru, hiyo ni kawaida yao katika kipindi chote cha mwaka, lakini kuna baadhi ya miezi na vipindi vya ziara maalum, miongini mwake ni mwezi wa Mwenyezi Mungu ambao thawabu huongezeka mara dufu, vitengo vyote vinashindana katika kutoa huduma, kuna huduma ambayo asilimia kubwa ya watumishi wanashiriki nayo ni kugawa chai kwa mazuwari ambapo huanza baada ya kufuturu hadi karibu na muda wa kula daku.
Kugawa chai usiku wa mwezi wa Ramadhani ni miongoni mwa utamaduni wa watu wa Karbala toka zamani, utamaduni huo ulipigwa marufuku baada ya maandamano ya Shaabaniyya ya mwaka 1991 kama zilivyo pigwa marufuku tamaduni zingine nyingi, utamaduni huu ulirudi tena mwaka 2003 na unaendelea hadi sasa, chai hii inamaandalizi maalum, huwekwa viungo pamoja na maji ya waridi kidogo na hupikwa kwa namna ya pekee, hupikwa katika moto mdogo mdogo wa kuni, chai hii inaradha nzuri watu wanaipenda sana, watu hutoka mbali na kuja kufuata chai hii pia kutokana na huduma nzuri yenye upendo wa hali ya juu wanayo pewa na watumishi, pia watu wanaokuja kufanya ziara huhesabu kua ni miongoni mwa khairaat za Abulfadhil Abbasi (a.s).
Imeandaliwa sehemu ya nje ya ukumbi wa haram ya Atabatu Abbasiyya tukufu karibu na mlango wa Alqamiy kwa ajili ya kugawa chai kwa mazuwaru, zoezi hilo linasimamiwa na jopo la masayyid watumishi wa Ataba tukufu na kitengo cha maukibu pamoja na watumishi wa vitengo vingine na watu wa kujitolea.
Kwa upande mwingine! Kitengo cha Maqaamu Imamu Mahdi (a.f) chini ya Atabatu Abbasiyya nacho kinagawa chai kwa watu wanaokuja kufanya ziara, huduma hiyo inafanywa na jopo la watumishi wa kitengo hicho, huduma hii ipo kila siku ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu imehuisha tamaduni nyingi zilizo kuwepo zamani katika Ataba tukufu za Karbala na kupigwa marufuku na utawala uliopita (wa Sadam), kwa utukufu wa Mwenyezi Mungu tamaduni hizo zimerudi upya katika mazingira bora zaidi.