Miongoni mwa maeneo yaliyo kombolewa na jeshi la serikali pamoja na Hashdi Sha’abi upande wa kulia wa mji wa Mosul, na kuanza kurudi hali ya kawaida kidogo kidogo baada ya kupotea hali hiyo kwa muda mrefu, familia za wakazi wameanza kurudi kidogo kidogo huku wengine wakiwa bado wapo makambini, kamati ya misaada katika ofisi ya Muheshimiwa Marjaa dini mkuu Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani (d.dh.w) imefunga safari kwenda kutoa misaada ili kuchangia kupunguza machungu yao.
Msafara wa kutoa misaada katika mwezi huu mtukufu (mwezi wa Ramadhani) umeondoka kufuatia maelekezo ya moja kwa moja kutoka katika ofisi ya Marjaa mkuu, na kufuatia mawasiliano na taasisi ya Ain ya kulea jamii bila kujali mazingira magumu ya hali ya hewa na kiusalama, hii ndio kawaida yao toka walipo anza kutoa misaada kwa wakimbizi, safari hii wametoa vikapu 2500 vya chakula.
Misaada hiyo wamepewa watu wa mji wa Nahiya na vijiji vinavyo uzunguka mji huo, ugeni ulipokelewa kwa furaha kubwa, na watu wote walionyesha heshima na upendo mkubwa kwa Marjaa mtukufu na wakaonyesha kuthamini misaada anayo toa katika miji iliyo kombolewa, wakamuomba Mwenyezi Mungu amzidishie kila la kheri.
Kumbuka kua misafara ya kutoa misaada inaendelea kwa mujibu wa ratiba iliyo andaliwa toka zamani, ya kwenda katika hema za wakimbizi au katika miji iliyo kombolewa, kwa ajili ya kuwapunguzia machungu ya maisha, na kuwaonyesha kua Marjiiyya ndio kimbilio pekee la wairaq wote wa tabaka zote, na kuondoa picha mbaya inayo hubiriwa na maadui.