Mwezi uliopendwa na Mwenyezi Mungu, akauteua kua ndio mwezi wa kuteremka kitabu chake kwa watu awapendao zaidi, na akakifanya kitabu hicho kua ni takaso na pambo la waja wake, mwezi wa Ramadhani ambao ndani yake imeteremshwa Qur’an ili kuja kurekebisha tabia za watu na kuwaongoza katika haki pamoja na kuwaepusha na adhabu katika siku isiyokua na kurejea nyuma, kitabu kilicho bambanuliwa aya zake ili watu wafahamu makusudio yake, kitabu cha Mwenyezi Mungu zinapo somwa aya zake utaona nyoyo za waumini zinajaa hofu na wanakua wanyeyekevu.
Uhusiano wa mja na Qur’an ni uhusiano wa kiibada, na mapenzi ya kuisoma na kuisikiliza hayahusishi umri, hawa hapa wazee hawaja zembea (acha) kuhudhuria! Huja kila siku kushiriki katika kisomo cha Qur’an kinacho fanyika ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), nao wameshikamana na jambo hili kwa miaka mingi, hufika mapema kabla ya kuanza kusomwa Qur’an tukufu ambayo huwavutia sana na hufatilia kwa mazingatio makubwa kila neno ndani ya Qur’an tukufu, masikio yao ni sikivu na akili zao pamoja na nyoyo hua na mazingatio wakiwa katika hali ya kutafakari na unyenyekevu.
Maahadi ya Qur’an katika Atabatu Abbasiyya tukufu imeandaa misahafu yenye maandishi makubwa yenye muonekano mzuri pamoja na vikalio vizuri kwa wasio weza kukaa chini kwa muda mrefu, vilevile wanazingatia kugawa muda wa kusoma kwa wasomaji ambapo husomwa juzuu moja kila siku kwa wakati mnasaba bila kuwachosha.
Kumbuka kua kisomo cha Qur’an Tartiil ni moja ya shughuli muhimu zinazo fanywa na Maahadi ya Qur’an katika Atabatu Abbasiyya tukufu ndani ya mwezi huu wa Ramadhani, jambo hili linafanywa kila siku ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), ambapo husomwa juzuu moja kila siku chini ya jopo la wasomaji mahiri, na hupata mahudhurio makubwa.