Majlisi za mawaidha na mafundisho ya kidini zafanyika kila siku ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) katika mwezi wa Ramadhani..

Maoni katika picha
Miongoni mwa ratiba iliyo andaliwa na Atabatu Abbasiyya tukufu inayo tekelezwa mchana na usiku ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani ni kufanya majlisi za kutoa mawaidha na mafundisho ya kidini kila siku jioni ndani ya ukumbi wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), kwa ajili ya kueneza tabia tukufu za kiislamu, na kufafanua baadhi ya mambo yaliyo tokea katika historia ya Ahlulbait (a.s), pamoja na kunufaika na siku za mwezi huu mtukufu.

Majlisi hizi hufanywa kila mwaka kwa kushiriki mmoja wa makhatibu na huendelea mwezi mzima (siku thelathini), na hufanywa baada ya swala ya Maghribi na Ishaa, mwaka huu majlisi hizi zimeendeshwa na Shekh Swaahibu Twaaiy, mihadhara yake mitukufu ilijikita katika kuelezea mwenendo sahihi ulio fundishwa na Ahlulbait (a.s) kwa ajili ya kupandisha bendera ya kiislamu, na kuhakikisha uislamu unaenea sehemu kubwa ya dunia, pia ndani ya majlisi hizo alizungumzia minasaba (matukio) makubwa katika nyonyo za wafuasi wa Ahlulbait (a.s), kama vile kufariki kwa bibi Khadija (a.s), kuzaliwa kwa imamu Hassan (a.s), kuuawa kishahidi kwa Amirulmu-uminina (a.s) pamoja na mengineyo miongoni mwa mambo yaliyo tokea ndani ya mwezi huu mtukufu, alielezea vilevile mambo yanayo husu Fiqhi, Aqida na Akhlaq kwa kuzingatia umuhimu wa mwezi huu mtukufu.

Kulikua na mahudhurio makubwa ya waumini, waliokuja kusoma wakiwa na matumaini makubwa ya kunufaika na utukufu wa mwezi huu pia wakitafajia karama za ndugu wa bwana wa mashahidi Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu iliandaa ratiba maalumu ya mwezi wa Ramadhani mtukufu, miongoni mwa vipengele vya ratiba hiyo ni kuendesha majlisi za kutoa mawaidha na maelekezo ya kidini ndani na nje ya ukumbi wa haram tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: