Kwa picha: Uhudhuriaji mkubwa wa waumini wanaofanya ziara katika malalo ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) katika usiku bora wa mwisho miongoni mwa siku za mwezi mtukufu..

Maoni katika picha
Katika usiku na mchana wa Ijumaa kuna A’amaali (ibada) nyingi, miongoni mwa ibada hizo ni kumzuru imamu Hussein (a.s), nalo ni jambo ambalo hupewa umuhimu na wafuasi wa Ahlulbait (a.s), usiku wa Ijumaa Karbalaa hua inaradha ya aina yake, hawezi kuihisi radha hiyo ispokua aliye bobea katika kumpenda imamu Hussein (a.s), sasa vipi utakapokua usiku huo upo ndani ya mwezi wa Mwenyezi Mungu mtukufu mwezi wa Ramadhani tena usiku wa mwisho ndani ya mwezi huo!.

Ataba mbili tukufu (Husseiniyya na Abbasiyya) baada ya Adhuhuri ya Alkhamisi tarehe 26 Ramadhani zilifurika waumini waliokuja kufanya ziara katika malalo ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s), watu walianza kumiminika katika maeneo haya matukufu Alasiri ya leo (Alkhamisi) na wameendelea kumiminika hadi wakati wa Maghribain chini ya usimamizi makini na ulinzi mkali wa usalama kutoka kwa watumishi wa Ataba mbili tukufu, ambao wamejitolea kuwahudumia mazuwaru na kuwapa vitu muhimu kama vile matandiko, maji baridi na kuhakikisha misahafu, vitabu vya dua na ziara vinapatikana kila sehemu, na wameandaa magari yanayo tumia umeme kwa ajili ya kubeba watu ndani ya maeneo ya Ataba za Karbala tukufu, na mabasi ya kawaida kwa ajili ya kupeleka na kurudisha watu katika vituo vya mabasi, pia wanagawa futari katika migahawa (mudhifu) yao, pamoja na kuandaa sehemu maalum katikati ya haram mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) na kugawa maji na barafu kabla la muda wa kufturu.

Ulipo karibia muda wa Maghribain walinyanyua mikono na kuomba dua kwa hisia na uchungu kutoka katika nyoyo za waumini na mazuwaru wakiiombea Iraq pamoja na wanajeshi wa serikali na Hashdi Sha’abi wanao onyesha ujasiri na ushujaa mkubwa katika kuwang’oa magaidi ya Daesh na kukomboa sehemu zilizo baki katika aridhi ya Iraq, wakitawasal kwa imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) wamemuomba Mwenyezi Mungu awape ushindi na awaponye haraka majeruhi wao.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: