Ofisi ya Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani (d.dh) yataja kiwango cha Zakatu-Fitri..

Maoni katika picha
Ofisi ya Marjaa dini mkuu Muheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani (d.dh.w) imetaja kiwango cha Zakatu-Fitri ya mwaka huu kua ni (1,500) dinari za kiiraq kwa mtu mmoja badala ya unga kwa mwaka wa (1438h).

Kiwango halisi cha Zakatu-Fitri ni pishi moja, ambalo ni sawa na kilo tatu za (chakula kinacho pendwa na watu wa mji husika) kama vile; ngano, zabibu, mchele, na zinginezo, au kutoa thamani yake, ni wazi kua thamani yake inatofautiana katika kila mji.

Inaitwa Zakatu-Fitri kwa sababu ni wajibu kutolewa katika siku ya Fitri, pia huitwa Zakatu-Abdaani (Zaka ya miili) kwa sababu inamlinda mtu na umauti na inamtakasa, inatofautiana na zaka nyingine kwa sababu hii imefaradhishwa kwa watu na sio kwa mali, yaani imefaradhishwa kwa ajili ya kutakasa nafsi za waliofunga na sio kutakasa mali kama ilivyo zaka ya mali, na watu wanaotakiwa kupewa Zakatu-Fitri ni mafakiri na masikini watu ambao ni halali kupewa zaka ya mali.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: