Matarajio ya kuandama mwezi wa Shawal mtukufu na sikukuu ya Iddul-Fitri..

Maoni katika picha
Inatarajiwa kuonekana mwezi siku ya Juma Pili jioni (29 Ramadhani 1438h) sawa na (25 Juni 2017m) na kunauwezekano wa kuuona kwa macho moja kwa moja katika anga la mji wa Najafu saa moja na dakika kumi na mbili (7:12) jioni wakati wa kuzama jua iwapo anga likiwa safi, kwa mujibu wa jeduali la mawio na machweo lililo sambazwa na ofisi ya Marjaa dini mkuu Muheshimiwa Ayatullah Sayyid Ali Husseini Sistani (d.dh.w) jaduali hilo linaonyesha kua:

Mwezi unatarajiwa kuandama siku ya Juma Pili jioni (29 Ramadhani 1438h) sawa na (25 Juni 2017m) katika anga la mji wa Najafu wakati wa kuzama jua saa moja na dakika kumi na mbili (7:12) ukiwa na umri wa saa (37) na dakika (37) na utakua juu ya usawa wa bahari kwa daraja (14) na dakika (8).

Unatarajiwa kuendelea kuonekana baada ya kuzama jua kwa muda wa saa moja na dakika (13) kiwango cha mng’ao wake ni (%3,59), unatarajiwa kuonekana wazi tena ukiwa juu.

Kutokana na matarajio haya, siku ya Juma Tatu (26/06/2017m) itakua siku ya kwanza ya sikukuu ya Iddul-Fitri tukufu, tunabaki wote pamoja tunasubiri kuandama mwezi kwa mujibu wa matarajio haya na kutangazwa kisheria kuanza kwa mwezi mtukufu wa Shawaal, Mwenyezi Mungu aurudishe tena mwezi mtukufu kwa baraka, rehema na maghfira.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: