Miongoni mwa mfululizo wa visomo vya Qur’an vinavyo endeshwa na kusimamiwa na Maahadi ya Qur’an tukufu katika Atabatu Abbasiyya, ni usomaji wa Qur’an Tartiil unaofanyika kila siku katika Maqaamu ya imamu Mahadi (a.f) ulio anza toka siku ya kwanza ya mwezi huu mtukufu hadi siku ya mwisho.
Qur’an husomwa kila siku baada ya swala za mchana (dhuhurain) na hushiriki wasomaji kutoka ndani na nje ya Maahadi ya Qur’an tukufu, hupata mahudhurio makubwa kutoka kwa watumishi na watu wanaokuja kufanya ziara, kila siku husomwa juzu moja, kwa usomaji wa ufuatiliaji baina ya msomaji na washiriki.
Kumbuka kua Maahadi ya Qur’an tukufu imeandaa ratiba maalumu ya kutekelezwa usiku na mchana ndani ya mwezi huu mtukufu wa Ramadhani inayo husisha vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni usomaji wa Qur’an na kubaini vipaji vya usomaji wa Qur’an pamoja na kuvilea, na kuangalia namna ya kunufaika kiroho kutokana na utukufu wa mwezi huu.