Kwa picha: Swala ya Iddi katika malalo ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na eneo la baina yao..

Maoni katika picha
Ndani ya eneo tukufu la malalo ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na eneo la baina yao, katika mazingira bora na nyoyo zilizojaa mapenzi ya Allah (s.w.t) na Mtume wake pamoja na watu wa nyumbani kwake (a.s), asubuhi ya siku ya Juma Tatu (1 Shawwal 1438h) sawa na (26 Juni 2017m) waumini wameswali swala ya Iddi katika eneo hilo iliyo ongozwa na Muheshimiwa Sayyid Murtaza Kazwini katika uwanja wa katikati ya haram mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) tukufu, swala hiyo ilihudhuriwa na waumini wengi sana miongoni mwa watu waliokuja kumzuru imamu Hussein (a.s) ambayo ni miongoni mwa ibada muhimu katika siku hii tukufu. Viwanja vya hafam ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) vimefurika watu wengi ambao hawajawahi kushuhudiwa walio jitokeza kuswali swala hii ya Iddi, hii inatokana na kuingia wageni wengi katika mji huu mtukufu kutoka ndani na nje ya nchi.

Wamejikurubisha kwa Mola wao katika swala zao na kumuomba; aujalie umma wa kiislamu na ulimwengu mzima amani na utulivu, na awapatie ushindi na utukufu wananchi wa Iraq, awalinde na njama za maadui, awafedheheshe maadui, ubaya wao uwarudie wenyewe, avunje umoja wao, ajalie bendera za wanajeshi wetu wa Iraq na Hashdi Sha’abi ziwe juu daima, awarehemu mashahidi wa Iraq na kuwaponya haraka majeruhi wao watukufu, kwa utukufu wa imamu Husseia na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s).

Kumbuka kua Ataba mbili (Husseiniyya na Abbasiyya) tukufu zimejipanga kuimarisha ilinzi na kutoa huduma maalumu katika siku hizi za sikukuu tukufu, zinatumia uwezo wao wote katika kuwapokea mazuwaru wa imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhakikisha wanapata huduma bora.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: