Maahadi ya Qur’an tukufu yakhitimisha ratiba yake ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya asifu na kupongeza juhudi zao katika swala la Qur’an..

Maoni katika picha
Sifa na pongezi kutoka kwa katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t), aipongeza Maahadi ya Qur’an chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu kwa kuendesha ratiba ya Qur’an ndani ya mwezi mzima ya Ramadhani, ratiba iliyokua na vipengele vingi vinavyo lenga kunufaika na mwezi huo mtukufu mwezi wa Qur’an, Maahadi hiyo ilijipanga mapema na kuandaa ratiba kabla ya kuingia mwezi wa Ramadhani, ratiba hiyo imepongezwa na kila mtu, kutokana na uzuri wa mpangilio wao na mpangilio wa Ataba tukufu.

Hafla ya ufungaji wa ratiba hiyo ilifanyika usiku wa Iddul-Fitri ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s) na kuhudhuriwa na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu ambaye alikua mfutiliaji mzuri wa ratiba hiyo, pia ilihudhuriwa na viongozi wengi na watumishi wa Ataba tukufu, wakiwemo watu walio shiriki katika usomaji wa Qur’an Tartiil na baadhi ya wawakilishi wa matawi ya Maahadi ya ndani na nje ya mkoa wa Karbala.

Baada ya kutolewa tamko la shukrani na mkuu wa Maahadi Shekh Jawaad Nasraawiy, zikatolewa zawadi kwa washiriki wa ratiba hii kwa kuanza na wale waliokua wasomaji wa Qur’an Tartiil iliyosomwa kila siku ndani ya mwezi wote wa Ramadhani, na wale walio shiriki katika mashindano ya Qur’an ya vikundi yaliyo pata mwitikio mkubwa, hali kadhalika wasimamizi wa ratiba hizo nao wakapewa zawadi.

Kumbuka kua ratiba ya Maahadi ya Qur’an tukufu ndani ya mwezi wa Ramadhani ilikua na vipengele vingi, miongoni mwa vipengele hivyo ni usomaji wa Qur’an Tartiil kila siku ndani ya uwanja wa haram ya Abulfadhil Abbasi (a.s), visomo vingine vya Qur’an tukufu viliendeshwa katika matawi ya Maahadi yaliyopo ndani na nje ya mkoa wa Karbala ikiwa ni pamoja na mashindano ya Qur’an, mahafali na ushiriki wa watoto katika usomaji wa Qur’an tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: