Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, kufuatia maelekezo ya uongozi wake mkuu kimepeleka shehena ya misaada mbalimbali ikiwa ni pamoja na chakula kwa wapikanaji watukufu wa Hashdi Sha’abi waliopo katika vizuizi vya utukufu na ushindi wakiendelea kuwatimua magaidi ya Daesh katika vitongoji walivyo kua wakivikalia magaidi hao ndani ya mji wa Mosul.
Kwa mujibu wa maelezo ya kiongozi mkuu wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu, msafara huu ulihusisha vitongoji vya: (Ba’aji, Tal-asfuuk, Hadhar na milima ya Sanjaar) vilivyopo ndani ya mji wa Mosul, msaada huu ni sehemu ya kutekeleza maagizo ya Marjaa dini mkuu aliye agiza kuwasaidia wanajeshi na Hashdi Sha’abi watukufu wanao pambana na magaidi ya Daesh na kuwatimua katika aridhi ya Iraq.
Misaada hii ni sehemu ya misaada mingi inayo tolewa na Ataba kwa wapiganaji wetu watukufu waliopo katika uwanja wa vita wanao jitolea kila walicho nacho kwa ajili ya kuihami Iraq na magaidi ya Daesh, tunaendelea kusimama pamoja nao hadi kukombolewa kwa ncha ya mwisho ya aridhi tukufu ya Iraq, upande wa kitengo cha habari na utamaduni, huu ni msafara wa pili na tunatarajia kuendelea misafara mingine kama hii.
Wapiganaji waliishukuru sana Atabatu Abbasiyya tukufu kutokana na juhudi yake ya kuwapa misaada mara kwa mara, wakasisitiza kua wako imara na wataendeleza ushindi hadi wahakikishe wameikomboa aridhi yote ya Iraq kutoka mikononi mwa magaidi ya Daesh.
Kumbuka kua Atabatu Abbasiyya tukufu hupeleka shehena za misaada ya vyakula na vitu vingine kwa vikosi vyote vya wapiganaji wa jeshi la serikali na Hashdi Sha’abi pamoja na kuunda kamati maalumu inayo simamia utoaji wa misaada kwa familia za mashahidi na kufuatilia kwa karibu hali za majeruhi.