Atabatu Abbasiyya tukufu haijafanya ajizi katika kutoa huduma ndani ya mji wa imamu Hussein (a.s) kwa kupendezesha maindhari yake, ukizingatia kua mamilioni ya watu kutoka ndani na nje ya nchi huja kufanya ziara katika mji huu, mradi wa kupanda miti unaofanywa na Atabatu Abbasiyya ni mmoja wa miradi muhimu kwa mji huu na watu wanaokuja kuutembelea, mradi huu unatoa matunda kwa kupendezesha hali ya hewa na kutoa vivuli kwa mazuwaru watukufu.
Mradi huu mtukufu ulianza miaka nane iliyopita, wataalamu wa Ataba wamefanikiwa kupanda miti katika maeneo mengi ya mji huu, miongoni mwa maeneo hayo ni: (kitongoji cha Iskaan, kitongoji cha Islaah, kitongoji cha Ta’aun, kitongoji cha Nasri, barabara ya Mkoa, barabara ya Hauliy, malalo ya Sayyid Judah, barabara ya Baabu Tuwaliji, barabara ya Maitham Tamaar.. na zinginezo nyingi, pamoja na barabara zote za mju wa zamani), imepandwa miti ya aina tofauti; kwa mfano: Kinu Karabsi, Baiziyya, Akasiyya, Surantis na miti ya mizaituni pamoja na aina zingine nyingi za miti inayo saidia kuboresha hali ya hewa kutokana na hali ngumu ya hewa hapa Iraq, hadi sasa kuna maelfu na maelfu ya miti iliyo oteshwa na kupandikizwa katika maeneo stahili kwa ajili ya kuboresha mazingira.
Kazi ya kupanda miti bado inaendelea hadi sasa katika barabara zote za mji mtukufu wa Karbala, tambua kua Ataba tukufu imechukua jukumu la kumwagilia na kutunza miti hiyo pamoja na kuilinda na maradhi mbalimbali, kupitia jopo maalumu la watalamu wa kitengo cha utumishi cha Ataba tukufu.