Atabatu Abbasiyya tukufu imetangaza kufaulu kwa mpango wake wa amani kwa kuwapokea na kuwahudumia watu waliokuja kufanya ziara Katika malalo ya imamu Hussein na ndugu yake Abulfadhil Abbasi (a.s) kutoka ndani na nje ya Iraq ndani ya mwezi mtukufu wa Ramadhani na siku za Iddul-Fitri, watumishi wa Abulfadhil Abbasi (a.s) walitoa huduma bora kabisa, kila mmoja alitoa huduma kulingana na kitengo chake na majukumu aliyo pangiwa, wote walifanya kazi kwa bidii chini ya lengo moja ambalo ni; Kumtumikia zairu aliye funga ni utukufu kwetu na ni kutafuta radhi za Mwenyezi Mungu na radhi za mwenye malalo haya Abulfadhil Abbasi (a.s).
Mwezi wa Ramadhani wa mwaka huu ulishuhudia mazuwaru wengi sana tofauti na miezi ya Ramadhani iliyo pita, juhudi ya kuwahudumia iliendana na idadi ya mazuwaru watukufu, watumishi wa Ataba walifanikiwa kuwapatia mambo yote muhimu na kuwawezesha kufanya ziara na ibada kwa urahisi, pia waliwapa huduma za chakula, vinywaji na vifaa vya kulalia pamoja na mambo mengine.
Huduma hizo ziliendelea hadi siku za Iddi (siku kuu), ambapo waliongeza huduma zaidi katika siku tatu za siku kuu ambazo zilikua na mahudhurio makubwa ya watu kuanzia swala ya Iddi mosi hadi siku ya Iddi tatu.