Mwaka wa tatu mfululizo Maahadi ya Qur’an tukufu kitengo cha wanawake katika Atabatu Abbasiyya chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu chapata nafasi ya kwanza katika mashindano ya Qur’an ya vikundi vya wanawake ya kitaifa yanayo simamiwa na Daru Qur’an ya Atabatu Husseiniyya tukufu kwa kushirikiana na “taasisi ya Baswaair” mashindano hayo yalifanyika ndani ya jengo tukufu la haram ya imamu Hussein (a.s).
Zilishiriki taasisi 16 za wanawake katika mashindano haya, kutoka katika mikoa tofauti ya Iraq, na walishiriki katika vipengele vyote; hifdhu, usomaji, tafsiri, maarifa ya Qur’an tukufu, fiqhi ya Qur’an pamoja na uwelewa wa Qur’an kwa ujumla, maswali yaliandaliwa na jopo la majaji wa kike walio bobea katika masomo ya Qur’an.
Kwa mujibu wa wasimamizi wa Maahadi ya Qur’an kitengo cha wanawake ndani ya Atabatu Abbasiyya, ushindi huu haukupatikana bure, ni matunda ya juhudi kubwa endelevu zinazo fanywa na viongozi wa kitengo hiki chini ya usimamizi imara wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu, ulio weka utaratibu mzuri na kuwaondolea vikwazo vyote kwa ajili ya kumtengeneza mwanamke bora aliye pambika na tamaduni za Qur’an, kufaulu katika mashindano haya ni dalili ya wazi ya juhudi kubwa iliyo fanyika.
Kumbuka kua mashindano haya ni sehemu ya ratiba ya wanawake (Rabii Quluub) iliyo andaliwa na taasisi ya Baswaair kwa kushirikiana na Daru Qur’an, ilikua na vipengele vingi na miongoni mwa vipengele hivyo ni mashindano haya.