Juma Tatu ijayo litaanza kongamano la Imamu Baaqir (a.s) la kitamaduni awamu ya tatu..

Maoni katika picha
Kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu kimetangaza kua Juma Tatu ijayo 08 Shawwal 1438h sawa na 03 Julai 2017m itaanza awamu ya tatu ya kongamano la imamu Baaqir (a.s) la kitamaduni chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir –a.s- ni kilele cha hekima na mfasiri wa wahyi) katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) ndani ya Ataba tukufu saa kumi na nusu alasiri.

Kwa mujibu wa maelezo ya mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano na naibu rais wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu Sayyid Aqeel Abdulhussein Yaasiriy, akaongeza kusema kua: “Awamu ya tatu ya kongamano hili ni muendelezo wa awamu mbili zilizo pita, tunatarajia awamu hii iwe ya aina yake, iendane na hadhi ya muhusika wa kongamano hili ambaye itazungumzwa historia yake; imamu Muhammad Baaqir (a.s) na kuelezea nafasi yake katika uislamu, kutokana na umuhimu wa zama za uimamu wake zilizo jaa tofauti za kiitikadi na namna alivyo simama imara katika kubainisha haki ukizingatia yeye ni mrithi wa elimu ya mitume (a.s), pamoja na kubainisha namna alivyo dhulumiwa kwa kuvunjiwa kaburi lake tukufu pamoja na makaburi ya maimamu wengine katika aridhi ya Baqii Gharqad”.

Akabainisha kua: “Atabatu Abbasiyya inautaratibu wa kufanya makongamano maalumu kwa maimamu waliozikwa Baqii (a.s), Imamu Hassan (a.s) kila mwaka hufanyiwa kongamano la kuzaliwa kwake tarehe kumi na tano ya mwezi wa Ramadhani, na imamu Sajjaad (a.s) hupewa nafasi maalumu katika kongamano la Rabiu Shahada, huku imamu Swaadiq (a.s) huadhimishwa pamoja na kongamano la Rabiu Risaalah au katika hafla za kitaifa za kumbukumbu ya kuzaliwa kwa muokozi wa walimwengu Mtume Muhammad (s.a.w.w), mtiririko wa makongamano haya hukamilishwa kwa kongamano la imamu Baaqir (a.s)”.

Akaongeza kusema kua: “Miongoni kwa faida za kongamano la kwanza lilifanikisha kuongeza katika maktaba jarida tatu zenye maudhui muhimu zilizo andikwa na waandishi mahiri wenye uzoefu wa muda mrefu na kuchapishwa, ilitokana na shindano la uandishi katika awamu hiyo, na katika awamu ya pili ilikua na washiriki wengi zaidi wa shindano la kitafiti, zimechaguliwa tafiti tatu zilizo pasi ambazo zitatangazwa siku ya ufunguzi wa awamu ya tatu ya kongamao hili.

Kuhusu ratiba na vipengele vya kongamano hili alisema kua: “Kongamano litakua na vipengele vingi miongoni mwa vipengele hivyo ni:

Kwanza: Ujumbe wa uongozi mkuu wa Atabatu Abbasiyya tukufu.

Pili: Qaswiga ya shairi la Amudiy.

Tatu: Maelezo kwa ufupi kuhusu walio faulu katika shindano la kitafiti la mwaka jana.

Nne: Qaswida ya shairi la Sha’abiy.

Tano: Ujumbe wa kamati ya maandalizi.

Sita: Maelezo kuhusu kongamano.

Saba: Kutoa zawadi kwa washindi wa tafiti na wanahabari walio shiriki katika kongamano”.

Kutakua na vipengele vitakavyo ongezwa katika kongamano vitatangazwa muda utakapo fika.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: