Tawi la Maahadi ya Qur’an katika jiji la Londan yafanya semina kubwa kuhusu maarifa ya Qur’an tukufu na kiongozi wake mkuu asema kua faida za semina hizi zimeanza kuonekana..

Maoni katika picha
Miongoni mwa mfululizo wa semina za Qur’an zinazo fanywa na tawi la Maahadi ya Qur’an chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu katika mji mkuu wa Uingereza Londan, imefanywa semina kubwa ya maarifa ya Qur’an chini ya uhadhiri wa Shekh Dhiyaau Dini Zubaidiy ambaye ni kiongozi mkuu (mudir) wa kituo cha maarifa ya Qur’an kuifasiri na kuichapisha –chini ya Maahadi ya Qur’an- na kiongozi mkuu wa sekta ya Qur’an tukufu.

Kwa mujibu wa maelezo ya Shekh Zubaidiy: “Simina hii ilikua na muitikio mkubwa, imehudhuriwa na walimu wengi wa Qur’an tukufu kutoka katika madrasa tofauti za kiarabu ndani ya Uingereza, huku walimu wengine wakishiriki moja kwa moja kupitia mitandao ya intanet (mtandao wa Skipe), uliwekwa utaratibu maalumu wa washiriki hao kwa kuyapa umuhimu zaidi mambo yanayo hitajika zaidi katika somo la maarifa ya Qur’an, na hatimae kuwatunuku vyeti kutoka katika Maahadi”.

Akasisitiza kua: “Semina zinazo endeshwa na tawi la Maahadi katika jiji la Londan zimesha anza kuzaa matunda katika uwanja wa Qur’an, kwa kuandaa washiriki na kuongezeka kiwango chao cha Qur’an pia wameweza kuakisi kwa vitendo katika ufundishaji wao, hakika semina hizi zimechangia pakubwa katika kuongeza kiwango cha elimu katika madrasa za Ulaya, haya yamefanikiwa kutokana na baraka za Abulfadhil Abbasi (a.s), haya ndio tulikua tukiyaomba na kuyatarajia toka kuanzishwa kwa tawi hili, tutaendelea kufanya harakati mbalimbali hadi tufikie malengo kwa ufanisi.

Kumbuka kua! Lengo la kufunguliwa tawi la Maahadi ya Qur’an tukufu katika jiji la Londan ni kwa ajili ya kutoa huduma za kielimu na masomo ya Qur’an chini ya mtazamo wa maimamu wa Ahlulbait (a.s) na kuifanya kua kiunganishi baina yake na Maahadi zilizopo katika mikoa tofauti ya Iraq, vilevile kua ndio mwanzo mwema wa kuendelea kufungua matawi mengine nje ya Iraq.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: