Baada ya kutengana na makazi yao: Kamati ya kusaidia wakimbizi katika ofisi ya Marjaa dini mkuu yaingiza furaha kwa watoto wa wakimbizi na mama zao katika mahema ya Hamaam Aliil..

Maoni katika picha
Kamati ya kusaidia wakimbizi chini ya ofisi ya Marjaa dini mkuu Muheshimiwa Sayyid Ali Husseini Sistani (d.dh.w) haijafanya ajizi katika kutoa misaada ya vifaa na chakula kwa familia za wakimbizi, wanapambana na mazingira magumu ya hali ya hewa na kukosekana kwa usalama wakati mwingine katika kutoa misaada, katika mnasaba wa Iddul-Fitri waligawa nguo kwa watoto wa kiume na wakike pamoja na wakina mama, wakaweza kuwapa furaha waliyo kua wameipoteza katika maisha yao kwa muda mrefu.

Kiongozi wa kamati inayo simamia ugawaji wa misaada ambaye alikuwepo katika ugawaji wa nguo hizo na hiyo ndiyo kawaida yake kusimamia kila tukio la ugawaji wa misaada, Sayyid Shaheed Mussawiy alisema kua: “Katika juhudi ya kutaka kuingiza furaha katika nyoyo za watoto na wakina mama wakimbizi katika mnasaba wa Iddul-Fitri, kamati imetekeleza maagizo ya ofisi ya Marjaa dini mkuu kwa kugawa nguo elfu tisa za wakina mama na watoto tulizo wapa familia elfu tatu za wakimbizi waliopo katika mahema ya Hamaam Aliil, aidha kuna aina zingine za zawadi tulizo wapa watoto kwa ajili ya kujaribu kuwapa furaha waliyo poteza, tuliona furaha katika nyuso zao wakati tukigawa zawadi hizo”.

Akaongeza kusema kua: “Ugawaji huo ulifanywa katika siku tatu za sikukuu (Iddi) na tulichagua mahema haya kwa sababu tuna picha kamili ya maisha wanayo ishi, kwani sisi tupo pamoja nao siku zote na tunajua mazingira yao, tunamshukuru Mwenyezi Mungu tumetekeleza jukumu tulilo pewa, sasa itafuata ratiba ya kwenda sehemu zingine kama ilivyo pangwa na kamati”.

Familia za wakimbizi walitoa shukrani kubwa kwa Marjaa dini mkuu Sayyid Sistani (d.dh) kwa misaada anayo wapa, inaonyesha wazi ukubwa wa utukufu wake na ubinadamu wa hali ya juu alio nao hakika yeye ni baba wa wairaq wote, kwa hekima yake tukufu ameweza kuitoa Iraq katika hatari kubwa iliyo tengenezwa na maadui wa ubinadamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: