Kamati ya maandalizi ya kongamano la Imamu Baaqir (a.s): kongamano linalenga kukumbusha tukio la Baqii na kuonyesha umuhimu wa kujengwa upya malalo haya matukufu..

Maoni katika picha
“Kongamano hili linalenga kukumbusha tukio chungu na kuamsha hisia kwa kila anaye unga mkono swala la kuyajenga upya malalo haya matukufu, tutaendelea kupaza sauti kwa namna yeyote ile, kuandika vitabu, Makala, tafiti, Qaswida, kufanya majaalisi na vinginevyo kadri tutakavyo jaliwa..”

Haya yalisemwa na Sayyid Aqeel Abdulhussein Yaasiriy mjumbe wa kamati ya maandalizi katika ujumbe alio wasilisha wakati wa kuhitimisha kongamano la imamu Baaqir (a.s), lililo fanyika alasiri ya Juma Tatu (8 Shawwal 1438h) sawa na (03 Julai 2017m) chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir –a.s- ni kilele cha hekima na mfasiri wa wahyi) ndani ya ukumbi wa imamu Hassan (a.s) katika Ataba tukufu.

Pia alibainisha kua: “Ni wazi mnajua umuhimu wa kuhuisha minasaba ya dini na kuienzi pamoja na kubainisha dhulma walizo fanyiwa Ahlulbaiti watakasifu (a.s), na miongoni mwa misiba mikubwa inayo umiza roho za wanadamu ni tukio la kuvunjwa makaburi ya maimamu wa uongofu na taa zing’aazo katika aridhi ya Baqii Gharqad, sehemu hii imebeba miili ya maimamu watakasifu na kundi kubwa la miili ya watu wa nyumba ya mtume (a.s)”.

Akasisitiza kua: “Uovu huu wa kinyama ni dalili ya wazi inayo onyesha haki na ukweli namna vinavyo fichwa na maadui wa ubinadamu na dini ya Mtume wa Rehema Muhammad na watu wa nyumbani kwake watukufu (a.s), inaonyesha maadui hao wa ubinadamu wanasikitika kwa kutokua pamoja na babu zao ili washiriki kuwaua na kuwateka watu wa nyumba ya mtume (a.s), hivyo na wao wameamua kuambulia kubomoa makaburi japo imepita mamia ya miaka, na kama wakipata nafasi zaidi wataendelea kuvunja makaburi mengine kama walivyo fanya watoto wao, kwa kuvunja malalo ya maimamu wawili (Askariyain) (a.s) na makaburi ya mawalii na waja wema mengine katika miji ya Iraq”.

Yaasiriy akaendelea kusema kua: “Sio rahisi kwao jambo hilo wakati kuna wanajeshi wenye roho imara kama chuma wanapata ilham kutoka kwa maimamu wao watakasifu na wanaitikia wito wa Marjaa dini wao mkuu, wako tayali kumshambulia kila anayetaka kuharibu nchi hii tukufu, wakasimama imara kulinda umoja na amani ya aridhi ya mitume, maimamu na mawalii (a.s)”.

Akasema kua: “Tufanye kila tuwezalo na waliyo fanya babu zetu pamoja na watakayo fanya watoto wetu hatuwezi kufikia hata asilimia kumi ya yale yaliyo fanywa na maimamu wetu watakasifu (a.s)”.

Sayyid Aqeel akamalizia kwa kusema kua: “Shukrani zote na utukufu umuendee kila aliye shiriki pamoja nasi katika kongamano hili, watu watukufu, watafiti, wageni, washairi, wana habari hususan waliosafiri hadi hapa, na shukrani za pekee zimuendee kiongozi mkuu wa kisheria wa Atabatu Abbasiyya Muheshimiwa Sayyid Ahmadi Swafi (d.i), pamoja na Muhandisi Sayyid Muhammad Ashiqar (d.t) katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya na wajumbe wote wa kamati kuu ya uongozi, bila kuwasahau marais wa vitengo na watumishi wote wa Ataba tukufu kwa juhudi zao na msaada wao mkubwa katika kufanikisha kongamano hili, na kwa namna ya pekee tunawashukuru kitengo cha habari na utamaduni pamoja na idara zake zote kwa namna walivyo tuo ushirikiano katika kufanyika kwa kongamano hili kama si wao pengine kongamano lisinge fanyika, bila kuwasahau Hashdi Sha’abi watukufu na jeshi la serikali kwani kama sio ushujaa wao na damu za mashahidi wao tusinge fanya kongamano hili wala tusinge weza kukutana na nyuso zenu tukufu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: