Kufuatia tukio la Baqii: Atabatu Abbasiyya yafanya kongamano la awamu ya tatu kuhusu imamu Baaqir (a.s)..

Maoni katika picha
Kufuatia kumbukumbu ya kila mwaka kuhusu kuvunjwa makaburi ya Baqii, alasiri ya Juma Tatu mwezi nane Shawwal sawa na tarehe tatu ya mwezi wa saba 2017 miladiyya lilianza kongamano la kitamaduni awamu ya tatu kuhusu imamu Baaqir (a.s), linalo simamiwa na kuendeswa na Atabatu Abbasiyya chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir –a.s- ni kilele cha hekima na mfasiri wa wahyi).

Kongamano hilo lilifanyika katika ukumbi wa imamu Hassan (a.s) ndani ya Atabatu tukufu, hafla ya ufunguzi ilipata mwitikio mkubwa sana kutoka kwa watu wa dini na wa kisekula pamoja na wawakilishi wa Ataba na Mazaru tukufu, na ilifunguliwa kwa Qur’an iliyo somwa na Haidari Jaluhani halafu ikasomwa surat Fat-ha kwa ajili ya kuwarehemu mashujaa walio uawa kwa ajili ya kulinda aridhi hii takatifu mashahidi watukufu wa Iraq.

Kisha ukafuata ujumbe wa Atabatu Abbasiyya tukufu uliowasiliswa na katibu mkuu Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t) ambaye alisema kua: (Kwa baraka za Mwenyezi Mungu mtukufu na neema zake kwetu, tunafanya kongamano la Imamu Baaqir (a.s) ambalo hua tukilifanya kila mwaka, mwaka huu tunalifanya chini ya kauli mbiu isemayo: (Imamu Baaqir –a.s- ni kilele cha hekima na mfasiri wa wahyi), ili tuweze kubainisha baadhi ya miongozo ya imamu huyu mtukufu, imamu wa tano katika maimamu wa Ahlulbait (a.s).

Baada ya hapo mshairi Aadil Swawiriy akapanda katika mimbari na kusoma shairi la amudiy ambalo lilizungumzia kudhulumiwa kwa imamu Baaqir (a.s) pamoja na maimamu wote walio zikwa Baqii.

Halafu wakatangazwa washindi watatu wa shindano la kitafiti, na walielezea kwa ufupi kuhusu tafiti zao:

Mshindi wa kwanza: Dokta Abbasi Ismaeel Al-gharawiy, utafiti wake ulihusu (Mwenendo wa imamu Baaqir katika namna ya kuishi kwa amani).

Mshindi wa pili: Ustadh Ali Abdulwahabi Al-ardawiy, utafiti wake ulihusu (Usomaji wa kisasa katika nukuu za kimalezi kutoka kwa imamu Baaqir –a.s-).

Mshindi wa tatu: Ustadh Rasul Muhammad Hassan Tamimi, utafiti wake ulihusu (Imamu Baaqir –a.s- na upatikanaji wa chuo kikuu).

Kipengele hiki kilihitimishwa kwa maswali na maoni yaliyo elekezwa kwa watafiti nao walitoa majibu na ufafanuzi pale ilipo hitajika kutolewa ufafanuzi.

Aidha mshairi Zainul-abidina Saidiy alisoma qaswida ya sha’abiy iliyo wakumbusha wahudhuriaji matukio ya Baqii ya uvunjaji wa makaburi matukufu, baada ya qaswida hiyo; naibu wa kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya ambaye pia ni mjumbe wa kamati ya maandalizi ya kongamano hili Sayyid Aqeel Abdulhussein Yaasiriy aliwasilisha ujumbe wa kamati ya maandalizi, miongoni mwa aliyo sema ni: “Kongamano hili linalenga kukumbusha tukio hili chungu na kuamsha hisia kwa kila anaye unga mkono swala la kuyajenga upya malalo haya matukufu, tutaendelea kupaza sauti kwa namna yeyote ile, kuandika vitabu, Makala, tafiti, Qaswida, kufanya majaalisi na vinginevyo kadri tutakavyo jaliwa..”

Kongamano lilihitimishwa kwa kutoa zawadi kwa washindi wa shindano la tafiti pamoja na kila aliye changia kufanikisha kwa kongamano hili ikiwa ni pamoja na wanahabari walio shiriki kutangaza kongamano hili.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: