Kamati ya maandalizi ya kongamano la kielimu la wanawake la kwanza lenye anuani isemayo: (Karbala ya pekee kwa uzuri na uwajibikaji) yatangaza mada za kitafiti zitakazo shindaniwa..

Maoni katika picha
Kamati ya maandalizi ya kongamano la kielimu la wanawake la kwanza litakalo fanyika chini ya kauli mbiu isemayo (Naihusia heri nafsi yako ewe ndugu yanngu) litakalo endeshwa na taasisi ya Waarithul- Anbiyaau Lidirasaati Takhasusiyya fi Nahadhatu-Husseiniyya (kitengo cha wanawake) chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu idara ya wanawake chini ya kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya, imetangaza mada zitakazo shindaniwa katika kongamano hilo kama zifuatavyo:

Kwanza: Mada za kifikra na kiitikadi.

  • 1- Nafasi ya mwanamke katika kujenga jamii yenye itikadi sahihi na fikra za muhanga wa imamu Hussein (a.s).
  • 2- Tukio la Karbala na athari chanya katika kukuza hisia za mwanamke kuhusu kudhulumiwa na kutenzwa nguvu.
  • 3- Nafasi ya mwanamke katika kuonyesha mateso na dhulma za tukio la Twafu.
  • 4- Upambanaji wa mwanamke kihistoria katika kuhuisha misingi ya muhanga wa imamu Hussein (a.s).
  • 5- Ukubwa wa imani katika maneno ya wanawake katika msafara wa imamu Hussein (a.s).
  • 6- Nafasi ya mwanamke kifikra katika kueneza misingi ya muhanga wa imamu Hussein (a.s) na malengo yake.

Pili: Mada za ki-akhlaqi na kijamii.

  • 1- Mwanamke Zainabiyya baina ya kujichunga na kutekeleza wajibu wake katika jamii.
  • 2- Matokeo chanya ya uwepo wa bi Zainabu katika msafara wa Imamu Hussein (a.s) na athari yake kwa watumishi na mazuwaru.
  • 3- Mtumushi wa kike! Mubalighah na nafasi yake katika kutangaza mafunzo ya dini kwa mazuwaru.
  • 4- Mtazamo wa jamii kidini kuhusu uwepo wa wanawake katika malalo matukufu na katika misimu ya mazuwaru wengi (mamilioni).
  • 5- Mtazamo wa kijamii katika kugawa majukumu baina ya wanaume na wanawake (msafara wa imamu Hussein) kama mfano.

Tatu: Mada za kilugha

  • 1- Utungaji wa mashairi kuhusu imamu Hussein (a.s) na uimbaji katikati ya wanawake.
  • 2- Nafasi ya fani za lugha kwa mwanamke katika kutangaza swala la imamu Hussein (a.s) na kulirithisha kwa vizazi vijavyo.
  • 3- Washairi kuathiriwa na mwanamke na nafasi yake katika tukio la Karbala.
  • 4- Ufaswaha wa mwanamke katika swala la imamu Hussein (a.s) na athari yake kwa wapokeaji.

Fahamu kua mwisho wa kupokea tafiti hizo ni Juma Tano ya tarehe 20/09/2017m, washiriki watafahamishwa kuhusu kukubaliwa ushiriki wao tarehe 15/10/2017m.

Tafiti hizo ziwasilishwe katika taasisi ya Waarithul-Anbiyaau chini ya Atabatu Husseiniyya tukufu katika ofisi zake zilizopo Najafu Ashrafu mtaa wa Hannaana, au kupitia anuani yake ya barua pepe: almarafikarbala@warithanbia.com pia unaweza kupiga simu: (07708730666 – 07813053831) au unaweza kuwasilisha katika Atabatu Abbasiyya idara ya wanawake kupitia barua pepe: library@alkafeel.net au piga simu namba: (07716199086 – 07826143083).

Kiongozi wa idara ya wanawake katika kitengo cha habari na utamaduni cha Atabatu Abbasiyya tukufu ameuambia mtandao wa kimataifa Alkafeel kua; kongamano hili miongoni mwa mambo muhimu linalo lenga ni:

  • 1- Kuchangia katika kuonyesha nafasi ya mwanamke kielimu na athari yake katika kufanikisha muhanga wa imamu Huseein (a.s) na malengo yake.
  • 2- Kuinua kiwango cha kutafakari cha watumishi wa kike katika Ataba na mazaru tukufu.
  • 3- Kudhihirisha uwezo wa kifikira na kitamaduni alio nao mwanamke na kusimamia itikadi yake katika misingi anayo iamini.
  • 4- Kuonyesha nafasi ya mwanamke katika kurekebisha jamii na mtu mmoja mmoja.
  • 5- Kubadilishana fikra na kuunganisha juhudi za wanawake wanao fanya kazi katika Ataba na Mazaru za kidini tukufu.
  • 6- Kusimama dhidi ya watu wanao shambulia na kujaribu kuharibu picha halisi ya mwanamke na kuzusha shubha katika dini tukufu ya kiislamu.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: