Pembezoni mwa mkutano ulio husisha waziri wa ulinzi Ustadh Arfaan Hiyaliy na mkuu wa kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) Ustadh Maitham Zaidiy, wametangaza kua jambo la kwanza ni kuungana rasmi kwa kikosi cha Abbasi na wizara ya ulinzi, baada ya kukamilika makubaliano muhimu ya kuwajumuisha wapiganaji wa kikosi hicho, walio pigana karibu miaka mitatu na bado walikua hawajaingizwa rasmi katika mfumo wa Hashdi Sha’abi.
Pande mbili zimekutana katika makao makuu ya Muheshimiwa waziri huko Bagdad na wamejadiliana mambo mengi ikiwa ni pamoja na swala la Tal-afar mji wenye umuhimu mkubwa.
Zaidiy akabainisha kua; wapiganaji wanaojumuishwa ambao wamekidhi vigezo vya kua wapiganaji wa kujitolea kwa mujibu wa wizara ya ulinzi watashiriki katika kutekeleza majukumu yajayo.
Vile vile Zaidiy ametoa shukrani nyingi kwa Muheshimiwa waziri kutokana na msaada mkubwa unao tolewa na wizara kwa wapiganaji wa kikosi cha Abbasi (a.s) ambao ndio sababu ya kuwafanya waendelee na kuimarika.
Tunapenda kuwafahamisha kua; kikosi cha wapiganaji cha Abbasi (a.s) ni moja ya vikundi vya wapiganaji wa kujitolea ambao wamesajiliwa chini ya mfumo wa Hashdi Sha’abi kikosi namba 26, nao ndio walio wakilisha Hashdi Sha’abi katika vita ya kukomboa upande wa kulia wa mji wa Mosul na waliweza kukomboa eneo kubwa la mji huo wakishilikiana bega kwa bega na jeshi tukufu la serikali ya Iraq.