Baada ya kushindwa moja ya hospitali ya kimataifa: Hospitali ya rufaa Alkafeel yarejesha jicho (uoni) wa mpiganaji ulio toweka katika vita ya kukomboa mji wa Mosul..

Maoni katika picha
Bado hospitali ya rufaa Alkafeel chini ya Atabatu Abbasiyya tukufu inaendelea kufanya kila iwezalo kwa ajili ya kurejesha furaha kwa wapiganaji wa serikali na Hashdi Sha’abi walio pata majeraha katika vita ya kukomboa aridhi za Iraq, wameendelea kufanya kazi kwa bidii chini ya maelekezo ya moja kwa moja kutoka kwa uongozi mkuu wa Ataba tukufu, tukio lililo tekelezwa na hospitali hivi karibuni ni moja kati ya matukio mengi makubwa ya kuokoa maisha au kurejesha kiungo yanayo fanywa na hospitali hii.

Majeruhi Kaadhim Faisal aliye fanyiwa upasuaji ni mmoja wa wapiganaji wa Hashdi Sha’abi, alipata jeraha kubwa katika jicho lililo pelekea kupoteza uoni kabisa, alikua amesha fanyiwa utafiti na hospitali nyingi za kimataifa zilizo mthibitishia kua ni vigumu kurejesha tena uoni wake, alipo ingia katika hospitali ya Alkafeel wataalamu wetu walio bobea katika sekta hiyo walijitahidi kumuokoa na kurejesha uoni wake aliokua amepoteza, baada ya kukamilisha vipimo vya lazima walimfanyia upasuaji kwa umakini na uangalifu wa hali ya juu kabisa ulio endeshwa na jopo la madaktari bingwa akiwemo daktari Khalidi Siraji.

Kwa mujibu wa maelezo ya dokta Siraji, upasuaji ulikua mgumu kulingana na jeraha alilo kua nalo, lakini baada ya kumtegemea Mwenyezi Mungu na kufuatia umahiri wa wataalamu wetu walifanikisha kazi hiyo, akabainisha kua “Hakika upasuaji huu ulikua hatari sana kutokana na jeraha kubwa alilokua nalo katika jicho lililo pelekea kupoteza uoni wake kabisa, lakini upasuaji umefanyika kwa mafanikio kutokana na vifaa tiba vya kisasa vinavyo milikiwa na hospitali pamoja na umahiri wa wataalamu wake”.

Majeruhi pamoja na ndugu zake wametoa shukrani za dhati kwa hospitali ya rufaa Alkafeel kutokana na huduma bora waliyo pata hali kadhalika juhudi kubwa iliyo fanywa na watumishi wa hospitali ambayo hailezeki.

Kwa maelezo zaidi kuhusu huduma zinazo tolewa na hospitali ya rufaa Alkafeel tembelea mtandao wetu wa: (www.kh.iq) au piga simu: (07602344444/ 07602329999).
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: