Kufutia kukubalika kwa hali ya juu: Mradi wa kiongozi wa wasomaji wa kitaifa waingia awamu ya tatu..

Maoni katika picha
Chini ya utaratibu mpya na kufuatia kukubalika kwake, kituo cha kuandaa wasomaji na mahafidhi katika Maahadi ya Qur’an tukufu chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu katika Atabatu Abbasiyya chaingia awamu ya tatu ya mradi wa; kiongozi wa wasomaji wa kitaifa –wa kuandaa na kulea vipaji- ambapo kutakua na washiriki kutoka ndani na nje ya mkoa wa Karbala baada ya kufanyiwa usaili na kukamilisha masharti yaliyo wekwa na kamati inayo simamia mradi huu.

Mradi wa Qur’an ni moja ya miradi mingi inayo fanywa na Maahadi ya Qur’an tukufu, unalenga kutengeneza jamii inayo jitambua na kufuata mwenendo wa Qur’an tukufu kwa kutoa mafunzo maalumu ya muda mfupi, kwa kusajili wanafunzi wa shule za msingi na upili (sekendari) kutoka katika mikoa mbalimbali ya Iraq, na kunufaika na kipindi cha likizo za majira ya joto (kiangazi) na kuhakikisha tunaandaa idadi kubwa ya wasomaji ambao watakua na kiwango kizuri katika kipindi cha miezi miwili takriban kwa awamu ya kwanza ya mradi huu.

Wakufunzi wa Qur’an wamegawana majukumu kwa kila halaqa ya Qur’an, kila halaqa itakua na mwalimu maalumu; na zitakua kama zifuatavyo:

  • 1- Madrasa ya Haafidh Khaliil Ismaeel/ Mkufunzi Sayyid Haidari Jalukhaan.
  • 2- Madrasa ya Muhammad Swadiq Minshawi/ Mkufunzi Muhammad Ridha Salmaan.
  • 3- Madrasa ya Abdulbaasit Muhammad Abduswamad/ Mkufunzi Ali Ahmad.
  • 4- Madrasa ya Shahata Muhammad Anuur/ Wakufunzi wawili, Wasaam Abdusaadah na Leeth Rahim.
  • 5- Hatua ya pili ya mradi/ Wakufunzi wawili, Faisal Madwar na Ahmad Badriy.

Mkuu wa kituoa cha kuandaa wasomaji na mahafidhi wa Qur’an katika Maahad ya Qur’an tukufu Sayyid Hassanain Halu siku za nyuma alibainisha athari inayo patikana kwa wasomaji kua: “Hakika miongoni mwa usia muhimu wa wasomaji wakubwa na wanachuoni wa fani hizi, ni kupambika na maadili mema, jambo hili linahitaji nasaha na maelekezo kutoka kwa maustadhi, na hili linatarajiwa kufanywa katika mradi huu kwa kila mshiriki Inshallah”.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: