Kituo cha turathi za Karbala chahitimisha semina ya uhakiki wa vifaa kale (makhtutwaat) awamu ya sita..

Maoni katika picha
Kituo cha turathi za Karbala chini ya kitengo cha maarifa ya kiislamu na kibinadamu chahitimisha semina ya uhakiki wa vifaa kale awamu ya sita kuhusu (Maimamu wa Baqii -a.s-), ambayo ni miongoni mwa semina ambazo hufanywa na kituo hiki katika mradi wa kuandaa wahakiki na kueneza utamaduni wa kuhakiki vifaa kale, kituo hiki ni maalumu kwa turathi za mji mtukufu wa Karbala.

Hafla ya kufunga semina ilifanyika katika jengo la imamu Haadi (a.s), imehudhuriwa na jopo la watalamu wa sekta hii pamoja na katibu mkuu wa Atabatu Abbasiyya Muhandisi Muhammad Ashiqar (d.t), katika ujumbe wake aliashiria nafasi ya Atabatu Abbasiyya katika kuenzi turathi na kusaidia wahakiki kuhifadhi turathi za Ahlulbait (a.s), akawashukuru washiriki wa semina hii akitarajia kua wamefaidika na semina na wataenda kutumia maarifa waliyopata, hali kadhalika akatoa shukrani kubwa wa wasimamizi wa semina, walimu na wahisani.

Dokta Ihsaan Gharifiy mkuu wa kituo cha turathi katika ujumbe aliotoa kwenye hafla hii amesema kua: “Iko wazi kwa watu wengi na maulamaa wa turathi za kishia kua; turathi za kishia zilitelekezwa kwa muda mrefu, kwa mujibu wa hustoria turathi zetu zimefanyiwa dhulma kubwa ya kuchomwa na kutelekezwa vitu vya msingi, hili linaonekana bayana tunapo angalia vitabu vikubwa tunakuta majina yao ndani ya vitabu hivyo lakini katika ulimwengu wa turathi hatuoni kitu cha kuwahusu watu hao, athari zao zimefutwa kutokana na chuki za kifikra na kimtazamo dhidi ya wafuasi wa Ahlulbait (a.s), mji mtukufu wa Karbala ni miongoni mwa miji iliyo athirika zaidi na kuvunjwa kwa turathi zake kwa miaka mingi sana”,

Akaongeza kusema kua: “Hivyo! Kuhuisha turathi hizi kuna umuhimu sawa na jihadi wanayo pigana Hashdi Sha’abi na jeshi la serikali katika uwanja wa vita, kalamu ni silaha kubwa kwa watu wanaotaka kufuta uwepo wa wafuasi wa madhehebu ya Ahlulbsit (a.s), inakua ni jukumu letu hususan kupitia kalamu za wahakiki kuandika uhakiki wa turathi zetu na kudhihirisha hazina ya nuru yetu katika muonekano bora zaidi, hivyo kituo cha turathi za Karbala kimejitolea kuandaa wataalamu watakao weza kufanya uhakiki wa turathi (vifaa kale) kupitia semina hizi”.

Mkufunzi dokta Zamaan Ubeid Wasaam Maamuriy alisema kua: “Katika semina mbili zilizo pita tulifanikiwa kupata vifaa kale vitatu, vitasambazwa kupitia maelezo ya kitafiti katika jarida la turathi za karbala, tunatarajia kufikisha kurasa mia moja hadi kukamilisha uhakiki huo ili kitolewe kitabu cha uhakiki, chini ya uandishi wa mwanachuoni wa Karbala aliye bobea katika Fiqhi, tunatarajia kuendelea kufanyika kwa semina hizi”.

Hafla ilihitimishwa kwa kugawa vyeti vya shukrani kwa wawezeshaji na vyeti vya ushiriki kwa maustadhi wanasemina.
Maoni ya wasomaji
Hakuna maoni
Kuweka maoni
Jina:
Nchi:
Barua pepe:
Kushiriki: